Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 August 2014
Monday, August 25, 2014

Barcelona yaanza vema La Liga.



Na Oscar Oscar Jr

Kulikuwa na mambo matatu ya msingi ya kutazama kwenye mechi ya Barcelona vs Elche, moja ni kuona mwanza wa kocha
Luis Enrique, pili ni kutazama kama Messi amerejea kwenye ubora wake na mwisho, ni kumshuhudia kinda Munir El Haddadi akifanya mambo.

Lionel Messi alifunga magoli mawili na kufanya utawala wa meneja mpya wa Barcelona, Luis Enrique, kuanza kwa kishidno walipowacharaza Elche 3-0 kwenye mechi ya kwanza ya La Liga Jana usiku.

Messi alidhihirisha kuwa bado yumo na kuondoa kabisa simanzi ya kupoteza fainali ya Kombe la Dunia akiwa na Argentina mwezi uliopita kwa kufunga mabao mawili maridadi.

Mechi hiyo ilisimama kwa dakika kadhaa baada ya paka mweusi kuvamia uwanja na kupelekea mpira usimame kwa muda mpaka pale alipokamatwa na kutolewa nje. 

Mechi hiyo pia ilishuhudia Javier Mascherano akitolewa nje kwa kadi nyekundu huku  Chipukizi Munir El Haddadi, 18 akifunga bao kwenye mchezo wake wa kwanza na kufanya uwanja ulipuke kwa shangwe pale alipopumzishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Pedro Rodriquez.

Miamba hao walitishwa kwa muda wakati Luis Enrique, pia wa Argentina, alipopata kadi nyekundu kwa kosa la kuzuia fursa wazi ya kufunga bao makusudi dakika chache baadaye. 

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!