Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 August 2014
Thursday, August 21, 2014

Barcelona itarudi tena kwenye ubora wake?


Na Oscar Oscar Jr

Baada ya msimu uliyopita kushindwa kutamba kwenye ligi kuu nchini Hispania na barani Ulaya,  klabu ya Barcelona watajitosa uwanjani kuwania taji hilo musimu huu wakiwa na nia ya kuwanyamazisha wakosoaji wao ambao wanaamini timu hiyo imefulia.

Moja kati ya sababu zilizopelekea klabu hiyo kutoka mikono mitupu kwenye michuano yote msimu uliopita ni kupungua uwezo kwa wachezaji wake watatu mahiri wa kikosi hicho ambao ni Xaiv Hernandez, Andres Iniesta na Lionel Messi.  


Nahodha wa zamani, Luis Enrique Martinez, alitawazwa kama kocha mpya wa timu hiyo baada ya aliyekuwa kocha Tata Martino kujiuzuru wadhifa wake. 

Enrique alipewa kitita kinono cha zaidi ya euro milioni 150 kutumika ili kuimarisha  kikosi chao.Tayari mshambuliaji Luis Suarez na kiungo Ivan Rakitic ni baadhi  ya majembe mapya yaliyotuwa pale Catalunia.

Christian Tello amekwenda kwa mkopo kwenye klabu ya Fc Porto, Cesc Fabregas akiondoka na kujiunga na Chelsea huku Alexies Sanchez akijiunga na Arsenal. 

Golikipa Victor Valdes na Carles Puyol nao wamemaliza mikataba yao, ujenzi wa Barcelona ya msimu ujao utakuwa chini ya Luiz Suares, Messi ambaye bado anauwezo mkubwa na Neymar Jr

Kitendo cha Barcelona kumaliza msimu uliopita bila taji lolote hakikuwahi kutokea kwa kipindi cha miaka sita. Bado Barcelona atahitaji kupambana na Real Madrid ambayo nayo imeongeza nguvu kwa kuwasajili James Rodriquez, Toon Kroos na Keyler Navas huku mabingwa watetezi Atletico Madrid nao wakijiimarisha kwa kufanya usajili wenye tija.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!