Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 March 2014
Friday, March 28, 2014

YANGA WAKO FIT KUWAVAA MGAMBO.



Kikosi cha timu ya Young Africans tayari kimeshawasili salama jijini Tanga mchana wa jana kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya maafande wa Mgambo JKT utakaopigwa siku ya jumapili katika dimba la Uwanja wa Mkwakwani na jioni ya leo timu imefanya mazoezi katika Uwanja wa shule ya Sekondari Galanos eneo la Nguvumali.

Young Africans ambayo katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya timu ya Tanzania Prisons iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 5-0, wachezaji wake wlikua wachangamfu sana mazoezini leo kila mmoja akisema wanapigana kutetea Ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo.

Kocha Mkuu wa Young Africans mholanzi Hans Van der Pluijm amesema vijana wake wanaonekana kumuelewa vizuri sasa na kuyashika vilivyo mafunzo yake na ndio maana matunda yameanza kuonekana katika michezo miwili iliyopita kwa timu kuweza kujikusanyia pointi 6 na magoli nane ya kufunga, huku safu ya ulinzi ikizuia timu pinzani kuziona nyavu zao.

Msafara wa watu 29 umefikia katika hoteli ya Central iliyopo barabara ya nane jijini Tanga ambapo ndipo Young Africans hufikia pindi inakua na michezo ya Ligi Kuu.
Wachezaji waliopo jijini Tanga ni :

Magolikipa: Juma Kaseja na Ally Mustafa "Barthez"

Walinzi: Mbuyu Twite, Juma Abdul, Oscar Joshua, David Luhende, Kelvin Yondani na Nadir Haroub "Cannavaro"

Viungo: Frank Domayo, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Nizar Khalfani na Athuman Idd "Chuji"

Washambuliaji: Emmanuel Okwi, Mrisho Ngasa, Saimon Msuva, Didier Kavumbagu, Jerson Tegete, Hamisi Kizza na Hussein Javu

taarifa hii ni kwa mujibu wa website ya klabu ya YANGA.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!