Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 March 2014
Thursday, March 27, 2014

KOMPANY:KAZI BADO KWA MAN CITY KUTWAA UBINGWA.


Kapteni wa Manchester City, Vincent Kompany, amedumisha matarajio ya uwezo wa timu hiyo kushinda ligi ya Premier ya Uingereza baada ya kikosi chake kuwaadhibu majirani zao Manchester United 3-0 Jumanne.

Ushindi huo uliwainua kufunga mwanya kati yao na Chelsea wanaoshikilia nafasi ya kwanza hadi alama tatu na mechi mbili za huku wakiwa na mechi 2 mkononi. 

Kompany alisisitiza bado ni mapema kuwavisha taji hilo huku mechi kadhaa zikisalia ikiwemo safari yao ya Jumamosi kumenyana na Arsenal katika dimba la Emirates. 

“Hii ilikuwa hatua moja tu na timu zingine zina ubora bado na hadi wakati ule tutazoa alama zote, sitakubali kuona kuwa ndo tumefika,” mlinzi  huyo wa Ubelgiji alinena.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!