Searching...
Image and video hosting by TinyPic
29 March 2014
Saturday, March 29, 2014

CHELSEA WAKAMATWA MKIA NA CRYSTAL PALACE.



Mbio za Chelsea kutwaa taji la ligi ya Premier ya Uingereza zilipata pigo Jumamosi pale viongozi hao walipolala 1-0 ugenini Crystal Palace huku nahodha wao, John Terry, akipata fedheha ya kuifunga timu yake. 

Huku Chelsea wakichakazwa kwa mara ya kwanza katika miaka 24 na Palace, mabingwa Manchester United walipata afueni baada ya juma la majonzi pale walipoilipua Aston Villa 4-1 huku mshambuliaji wa Uingereza, Wayne Rooney, akipata magoli mawili. 

Terry alitia krosi ya Joel Ward wavuni mwao dakika ya 56 kwa kichwa ingawa tetesi zinasema mpira huo uligusa mkono wa beki wa Palace, Joe Ledley, kabla ya kutua kimyani.
Licha ya kulala, Chelsea walihifadhi uongozi na alama 69 lakini wapinzani wao katika harakati za kuwania taji hilo, Liverpool, ambao wanafuata alama moja pekee nyuma yao watatua kileleni ikiwa wataibwaga Tottenham Hotspurs Jumapili. 

Mabao kutoka Jay Rodriguez, aliyefunga mawili, Rickie Lambert na Adam Lallana, wote wa Uingereza, yalisaidia Southampton kuiadhibu Newcastle 4-0 huku Jonathan de Guzman akipata mawili na Wayne Routledge wakiongoza Swansea kuibwaga Norwich City 3-0 kwingineko. 

Straika wa Nigeria, Peter Odemwingie, aliendeleza makali yake tangu kujiunga na Stoke City baada ya kufunga bao la kipekee kwenye ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Hull City nao Cardiff wajinusuru baada ya kulazimisha sare ya 3-3 ugenini West Bromwich Albion huku vilabu hivyo vikipigana kusalia katika ligi ya Premier.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!