Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 March 2014
Friday, March 28, 2014

BAYERN NA PEP GAUDIOLA NI MWENDO WA REKODI TU.




Baada ya kushinda taji la Bundesliga, Bayern Munich sasa wanaweza kuanza kufikiria kushinda ligi bila kushindwa na kumaliza na alama za juu zaidi kuwahi kuzolewa na timu kwenye ligi hiyo.
Borussia Dortmund na Schalke wanapigania nafasi ya pili, huku vita ya kukwepa shoka la kushuka daraja ikiendelea kwa kuhusisha  timu saba wakiwemo mabingwa wa zamani Stuttgart na Hamburger SV. 


Bayern, ambao tayari wameshinda kombe la ligi mapema zaidi katika historia ya ligi hiyo, wanaweza kuvunja rekodi waliyoweka msimu uliopita walipomaliza na alama 91. 

Bayern kwa sasa wana alama 77, wakiwa na mechi saba zilizosalia ambapo wanaweza kutwaa alama 21. Bayern wameshinda mechi 25 kati ya 27 walizocheza, na kutoka sare mbili. 

Wameshinda mechi zao 19 za hivi karibuni na hawajashindwa katika mechi 52.Timu hiyo ya Pep Guardiola imo njiani kurudia ushindi wa mataji matatu msimu mmoja kama msimu uliopita, waliposhinda Bundesliga, Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na German Cup. 
 
Bayern watakutana na Hoffenheim mechi ijayo. Hoffenheim ambao wamekuwa wakifunga mabao mengi na pia kufungwa mabao mengi, wana safu ya pili kwa ubora katika kushambulia nyuma ya Bayern, na ambayo wamefunga mabao 60. Pia ina safu ya ulinzi bovu zaidi ambayo imefungwa mabao 59 kwenye ligi. 

Kipa wa Bayern Manuel Neuer anasema Bayer hawatatulia: “Huwa hatupotezi msukumo wetu. Tutamkabili kila mpinzani vikali na huwa tunaingia kwenye mechi tukiwa na imani kuu.” 


Stuttgart, mabingwa wa Bundesliga 2007, ni wa pili kutoka nyuma, wakiwa alama mbili kutoka eneo salama, baada ya kuchapwa 2-0 wakiwa Nuremberg katikati ya wiki. Sasa watakutana na Dortmund, ambao wako alama moja pekee mbele ya Schalke wakipigania nafasi ya pili. 

Chini ya kocha mpya Huub Stevens, Stuttgart waliilaza Hamburg lakini wakashinda Nuremberg na watalazimika kutafuta angalau alama moja dhidi ya Dortmund, ingawa ni kibarua kigumu kwao. 


Baada ya kwenda mechi tisa bila ushindi wowote katika mashindano yote na kushinda mechi tano kati ya sita walizocheza za Bundesliga, Leverkusen walijikwamua kwa ushindi wa 3-1 wakiwa Augsburg na labda wakamuokoa kocha Sami Hyypia. 

Leverkusen sasa wako alama tatu salama nambari nne, ambayo ina maana kwamba watafuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, na wako alama nne nyuma ya Schalke walio wa tatu. 

Hyypia alibadilisha kikosi chake cha kwanza nabado haijabainika kama nahodha Simon Rolfes atarejea kikosini dhidi ya Braunschweig inayoshika mkia, na ambayo iliangukia bahati kwa kuwalaza Mainz 3-1.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!