Searching...
Image and video hosting by TinyPic
26 March 2014
Wednesday, March 26, 2014

ARSENAL SASA KUISAKA TOP FOUR NA SIO TAJI TENA!

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ni kama amekiri kwamba hawawezi kushinda ligi na ameonya kuwa sasa wanalazimika kuangazia kumaliza katika nne bora baada ya kulazimishiwa sare ya 2-2 nyumbani na Swansea City kwenye Ligi ya Premia Jumanne. 


Vijana hao wa Wenger walianza wiki moja iliyopita wakiwa miongoni mwa wanaopigania taji lakini wameteleza baada ya kutwangwa 6-0 na viongozi Chelsea mechi ya 1 000 Wenger akiwa meneja wa timu hiyo Jumamosi na sare dhidi ya Swansea iliyotokana na bao la kujifunga dakika za mwisho lake Mathieu Flamini. 

Arsenal sasa wako alama sita mbele ya Everton walio wa tano, ambao walilaza Newcastle 3-0 Jumanne na wana mechi ambayo hawajacheza, huku wakipigania nafasi ya kushiriki Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.
"Kushinda taji si hofu kubwa kwetu sasa,” Wenger aliambia kikao cha wanahabari. 

“Lazima tuongee ukweli. Lazima sasa tutazame nyuma yetu. Everton walishinda, na bila shaka, sasa lazima tungazie mechi yetu ijayo (nyumbani dhidi ya Manchester City). 

"Manchester City walipata matokeo mazuri leo usiku (ushindi wa 3-0 Manchester United). Wanaonekana kuwa moto. Wao na Chelsea ndio wanaopigiwa upatu sasa kushinda taji. Hatuna nafasi sasa ya kurudi mbioni. 

Chelsea wana alama 69 kutoka kwa mechi 31 mbele ya City walio na alama 66 kutoka kwa mechi 29, huku Liverpool wakiwa nambari tatu na alama 65 kutoka mechi 30, Arsenal wa nne na alama 63 kutoka mechi 31 nao Everton alama 57 kutoka kwa mechi 30.

Nafasi ya Arsenal eneo la kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya inaonekana kuwa hatarini zaidi ikizingatiwa kwamba Manchester City watatua The Emirates Jumamosi kabla ya vijana hao wa Wenger kwenda Everton Aprili 6. 

"Matokeo hayo yanavunja moyo,” alisema Wenger. “Tukiwa 2-1 labda tuliogopa sana kwa sababu kujiamini kwetu kuliathiriwa na matokeo ya Jumamosi na tulitaka kushinda tu mechi bila kujitokeza sana na kushambulia.”
"Kosa lilitendeka na likapelekea matokeo ambayo hatukuyataka usiku huu.”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!