Na Oscar Oscar Jr
Katika watu wenye furaha siku ya leo,ni fans wa Liverpool.Baba
Delphina,mr Hat-trick,komando Suarez amekubali kusaini mkataba wa
kuitumikia Liverpool kwa miaka 5 ijayo!
Suarez ni mchezaji
anayestahili UCL ili iwe rahisi pengine kuelekea kwenye Ballon
D'or.Liverpool wanatakiwa kumuongezea nguvu.safu ya ushambuliaji,sina
tatizo nayo.
Liverpool inamuhitaji
mtu mmoja wa aina ya Alex Song au Luiz Gustavo ili kutuliza
dimba,inahitaji mtu mwingine wa aina ya Coutinho ili acheze sehemu ya
Gerrard ambayo naona jua lake liko machweo!
Lucas sio mzuri
sana,Handerson simkubali kabisa kama SAF na Allen,alitakiwa awe kwanza
stoke city.Wakipata aina ya Mata au Modric kucheza nafasi ya
Gerrard,gari la manzese litakuwa limewaka.
Kwanamna wanavyomvumilia Brendan Rodgers,atawajengea timu bora hivi punde.
21 December 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment