Searching...
Image and video hosting by TinyPic
12 November 2013
Tuesday, November 12, 2013

SINA MASHAKA HATA KIDOGO NA SAFARI YA KASSEJA JANGWANI.

NIONAVYO MIMI MTOTO WA TABORA:

SINA MASHAKA HATA KIDOGO NA SAFARI YA KASSEJA JANGWANI.

Na Oscar Oscar Jr


Golikipa Juma Kasseja na mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngassa ni aina ya wachezaji ambao mapenzi yao kwa Klabu za Karia koo huwa yanawapa sana wasiwasi wapenzi wa timu hizo.Pamoja na kuwa Mrisho Ngassa alichezea msimu uliopita  klabu ya simba,wana msimbazi hawakumuamini na sasa Juma kasseja anarejea Yanga kwa mara nyingine na ile dhana ya mashabiki wa Yanga iko pale pale.

Mrisho Ngassa na Juma Kasseja wanaponzwa na kitu kimoja tu,kuweka mapenzi yao hadharani basi.Inasadikika kuwa Juma kasseja anaipenda sana timu ya simba na Mrisho Ngassa anaipenda sana timu ya Yanga.Kuipenda timu sio tatizo hata kidogo,mshambuliaji wa klabu ya Arsenal,Theo Walcott tangu akiwa mtoto mdogo ni shabiki mkubwa wa timu ya Liverpool na akikutana na Liverpool huwa anawafunga magoli kama kawaida.


Ukimuuuliza Steven Mazanda wa timu ya mbeya city anashabikia timu gani na akikujibu anaipenda timu ya Yanga,hili sio kosa au ukimuuuliza Themi Felix wa Kaagera sugar na akakujibu kuwa anaipenda sana klabu ya Simba,mimi sioni tatizo na ndiyo maana mwanamuziki wa kizazi kipya toka Morogoro Stamina amewahi sema "unaweza ukawa shabiki wa simba na ukaishi mwembe yanga"


Juma Kasseja hakuongezwa mkataba na klabu ya Simba si kwa sababu ya umri wala kushuka kiwango,ni siasa zinazoendesha klabu ya Simba ndiyo chanzo cha yeye kutemwa na upande wa pili,Klabu ya Yanga nao wamemsajili kwa pesa nyingi sana pengine kuliko umri wake na kiwango chake ni kwa sababu za siasa hizo hizo zinazoendesha klabu ya Yanga!!

Anyway,mashabiki wanatakiwa kuelimishwa ili wajue kwamba,unapochezea YANGA sio lazima uwe shabiki wa timu hiyo.Hivi unadhani NIYONZIMA ni shabiki wa YANGA? unadhani TAMBWE ni shabiki wa SIMBA? Mwacheni kasseja akafanye kazi Yanga,kuipenda timu au kutokuipenda ni maisha yake binafsi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!