Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 November 2013
Saturday, November 16, 2013

KARIBU HASSANI DILUNGA JANGWANI.

NIONAVYO MIMI:YANGA WAKO SAWA KABISA KWA USAJILI WAO.


Na Oscar Oscar Jr 0789-784858,0769-282918
Klabu ya Yanga ikosawa Kumsajili Juma Kasseja,wako sawa kabisa Kumsajili Hassani Dilunga.Kasseja bado ni moja ya makipa bora Tanzania,Dilunga ni moja ya mafundi bora VPL na Yanga nayo ni moja ya klabu bora VPL.so wote ni bora!

Ni kweli yanga wanaongoza ligi lakini ni wazi kwamba,matarajio ya mashabiki wao yalikuwa makubwa kuliko kile Yanga walichokionyesha.Yanga hawaui vipaji,wachezaji wanajiua wenyewe!

Wadau wanaamini kwenda Yanga ni kuuwa kipaji,binafsi siamini hilo.Bahanuzi na wenzie wanaoozea benchi wamepewa sana nafasi kung'aa na Yanga lakini siku zote wanacheza chini ya kiwango!!

Yanga ni mahali ambapo kuna mafundi wengi kwa hiyo ni lazima pia uwe fundi ili upate nafasi.Dilunga akilewa sifa ni kweli,atakwenda benchi.Kasseja akicheza "ki-Joe Hart" ni kweli atakwenda benchi.

Wachezaji wengi ndoto zao ni kucheza Simba au Yanga na wakishafika hapo badala waendelee kulala ili waote kwende nje au kufanikiwa zaidi,wao wanaamka! Ushaona ndoto inaendelea ukiwa macho?

Ukiondoa wageni pale yanga,wachezaji wengi wa kibongo wanacheza "ki-father" hii ndiyo nafasi ya Dilunga ya kufanya kazi kama punda ili kuonyesha tofauti ya wao na yeye.

Namtakia kila la kheri Kasseja,namtakia kila la kheri Dilunga.

I'm sorry!

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!