Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 August 2013
Tuesday, August 06, 2013

MOYES: "SIHITAJI KUMSHAWISHI WAYNE ROONEY AU MCHEZAJI YOYTE KUICHEZEA MANCHESTER UNITED"


Huku tetesi mpya zikizuka kila siku juu ya hatma ya mshambuliaji  Wayne Rooney, kocha wa Manchester United David Moyes amesema jana Jumanne kwamba hahitaji kumshawishi mshambuliaji aendelee kubaki Old Trafford.
Alipoulizwa kuhusu namna Wayne Rooney alivyolipokea suala la United kukataa ofa mpya ya Chelsea ya £30m kwa ajili kumsajili, Moyes alisema, "Sijui, sijamuuliza kuhusu suala hilo."


Pia wakati akijibu swali la kama atamshawishi nyota huyo wa England aendelee kubaki kuitumikia klabu hiyo inayojinadaa kutetea ubingwa wake wa EPL, Moyes alisema: "Huhitaji kumshawishi mtu yoyote kuichezea Manchester United."
Moyes alikuwa akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo wa kirafiki ulioisha kwa sare ya 1-1 dhidi ya AIK jijii Stockholm.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!