Searching...
Image and video hosting by TinyPic
11 July 2013
Thursday, July 11, 2013

NIONAVYO MIMI BADO TUNAHITAJI KUBADILIKA NA INAWEZEKANA TU.



Leo nimepata fursa ya kutembelea mitaa mbali mbali ya jiji la MBEYA na kikubwa nilichokiona ni bendera kibao za simba na yanga zikipepea mitaa mbalimbali ya jiji hili.Ukipita madukani ndo balaa,kadi,jezi za simba na yanga ndo habari ya mujini.

Nilimejiuliza maswali mengi ambayo sikupata majibu,kwa nini hawapeperushi Bendera za MBEYA CITY ambayo msimu ujao itashiriki liki kuu Tanzania? kwa nini hawauzi jezi za timu ya Prison iliyoshiriki ligi kuu msimu huu uliomalizika?

Hatuwezi kupiga hatua kama kila siku,mawazo na akili zetu zitaendelea kutawaliwa na timu za SIMBA vs YANGA tu.Nikweli timu hizi lazima ziwe na mashabiki wengi nchini kutokana na mafanikio na historia ya soka nchini lakini,ninachokiona ni hapa kuna uwezekanao mkubwa wa ASTON VILLA ya uingereza kupata mashabiki wengi TANZANIA kuliko MBEYA CITY kuwa na mashabiki wao ambao hawako upande wa simba wala yanga.

Kwanamna ninavyoona MBEYA CITY watapata mashabiki wengi wa mkopo toka yanga siku watakapocheza na simba na kinyume chake.Nadhani hii tabia inatakiwa pia ife ili mambo mengine yaendelee.simba na yanga zenyewe presha tupu hamna chochote cha maana.

ngoja nichukue zangu jaketi,maana baridi la huku ni balaa ingawa nawaona jamaa hapa nje wamevaa kata mikono.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!