Searching...
Image and video hosting by TinyPic
12 June 2013
Wednesday, June 12, 2013

TETESI ZA USAJILI | MAROUANE FELLAINI, ARSENAL, CHELSEA, MAN UNITED



Kama ni mbio basi Arsenal wanaonekana ndio wanaongoza katia msururu wa klabu kubwa za EPL zinazomuwania kiungo wa Everton Marouane Fellaini.

Inawaje, pesa ndio inaweza kua ishu. Mchezaji huyo ana ada ya uhamisho £23million kama kifungu cha kuachana na Everton na kujiunga na klabu itakayoweza kutoa fedha hizo, ambazo bozi wa The Gunners Arsene Wenger anaona kama ni nyingi kulinganisha na thamani halisi ya kiungo huyo.

Huku Chelsea na Manchester United wakiusoma mchezo wakisubiri kwa hamu, Bosi wa Arsenal anatakiwa kufanya maamuzi ya haraka na kutoa pesa hizo ili kumnyakua kiungo huyo.

Kama Arsenal wakiendelea kupepesa macho, basi bosi wa zamani wa Fellaini aliyefanya nae kazi wakiwa Everton, David Moyes, atafurahi kumleta Old Trafford.

Jose Mourinho nae anamtamani kiungo huyo mwenye nguvu kama mbadala wa viungo wepesi wachezeshaji Stamford Bridge kwani anajaribu kubalansi timu kuwapa uhuru zaidi Mata na Oscar kuweka fikra zaidi kwenye ushambulizi msimu ujao.

Midfilda wa Everton anawavutia Chelsea, Manchester United na Arsenal, lakini ni The Gunners ndiye hasa angependa kusaini.
Swali ni kwamba - Je Arsenal watatoa kiwango kinachotakiwa kumuweka huyu kujiunga nayo?

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!