Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 June 2013
Sunday, June 30, 2013

NIONAVYO MIMI YA LEO INAMUHUSU KATIBU MKUU WA TFF


Alhamisi wiki hii nilikuwa mmoja kati ya watu 25 waliokutana na katibu mkuu wa TFF na kumsikiliza kwa makini kabisa wakati alipokuwa akichangia kueleza matatizo ya soka nchini na kupendekeza njia za kuyatatua.

1.Angetile alianza kueleza tatizo la makocha ambapo alisema nchi yetu inamakocha wacheche sana ambao wamesomea ufundishaji wa mpira na waliowengi wanafundisha kwa uzoefu tu na sio taaluma.sababu ya kuwa na makocha wachache,Angetile alisema ni pamoja na watu kutokuwa na elimu ya kidato cha 4.

2.Angetile aligusia pia tatizo la marefa ambalo pia linakwenda sambamba na makocha,kigezo cha elimu kimeendelea kuwaangusha wengi kwani ili uweze kusoma kozi hizi ni lazima angalau uwe na cheti cha kidato cha 4.

3.Angetile aliweza pia kueleza kwamba makocha wengi wa mtaani ambao hawajapewa mafunzo ya kisasa,wamekuwa na tabia ya kuwapa wachezaji mazoezi magumu ambayo kwa kiasi fulani yanasababisha baadhi ya vijana kukwepa mazoezi na kuuchukia kabisa mchezo wa soka.

4.Mapendekezo yake,Serikali inatakiwa kushusha bei vifaa vya michezo na pengine kuvipeleka mashuleni bure kabisa ambako ndiko wanakopatikana wachezaji wengi.Waalimu wa shule wapewe mafunzo ya ukocha na urefa kwa sababu Elimu wanayo.Serikali itenge maeneo ya viwanja na kuyaboresha ili watu wengi wapate fursa ya kuendeleza vipaji vyao.

5.Angetile amesema waalimu wa shule ndiyo wanaanza kukaa na wanafunzi na nidhahiri kwamba wao ndo chanzo cha kutambulisha vipaji vya watoto lakini pia lazima wapewe ushirikiano na wazazi na serikali kwa ujumla.

kwa kuhitimisha,katibu mkuu huyu wa TFF amesema wasomi ni vema wakaona fursa nyingi zilizopo kwenye mchezo wa soka na kuzitumia kwa manufaa ya Taifa letu na watu wenye kipato,wasisite kuwekeza katika soka na michezo kwa ujumla kwa sasa inalipa.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!