Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 June 2013
Tuesday, June 25, 2013

NIONAVYO MIMI KWENYE LUGHA YA KIINGEREZA VS SOKA



Kiingereza ni moja kati ya sababu kibao zinazofelisha wadogo zetu shuleni.Makocha wengi wa timu za Simba,Yanga na Azamu na wale wa TAIFA STARS wamekuwa ni watu ambao hawajui kiswahili.Hivi huwa hakuna tatizo kama la kwenye sekondari zetu wanapokuwa mazoezini?

Jose Mourinho pamoja na Ureno wake,kiingereza anajua.Arsene wenger pamoja na ufaransa wake,kiingereza anajua na Roberto Martinez pamoja na uhispania wake,kiingereza anajua.Hivi Kim Poulsen muda wote huu hajui kiswahili au hataki?

Wachezaji wetu wa siku hizi naskia eti wanasoma tuition ya kiingereza,kama mtu anasoma mpaka PHD na bado anachemka kwenye kuongea hicho kizungu,itakuwa wewe unaye jifunza kwa miezi 2?

Pep Gaudiola wakati anahusishwa kuja chelsea,ilisemekana alikuwa marekani anajifunza kiingereza.Hivi kwa nini tusimpeleke kocha tu akajifunze KISWAHILI FASTA badala ya wachezaji wetu wote kwenda English course?

Hawa kina maximo na wenzake wanaamini kama kiingereza kinaeleweka kote duniani,wanasahau kama huku kwetu minara ya MTANDAO wa kiingereza iko chini.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!