Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 June 2013
Friday, June 07, 2013

MUNGU IBARIKI TANZANIA


NIONAVYO MIMI HADI HAPA TULIPOFIKA,TUMEFANYA VIZURI


Katika ukanda wa Africa Mashariki ni Tanzania tu ndo bado inauwezo wa kusonga mbele kwenye kufuzu kwa hatua ya kwanza ya mchujo wa kushiriki kombe la Dunia BRAZIL MWAKANI.

Tanzania inashika nafasi ya 2 ikiwa na points 6 nyumba ya Ivory Coast wanaongoza kundi hilo wakiwa na points 7.Wengine ni Moroco wenye points 2 na Gambia wakiburuza mkia wakiwa na points 1.

kama Tanzania itashinda mechi dhidi ya Moroco ambayo binafsi naiona ngumu kuliko hata ya Ivory coast,itaongeza morali na ujasiri wakuona kwamba "yes we can" na kuanzia hapo kazi itakuwa moja tu,kuja kuwasambaratisha Ivory coast kwenye uwanja mkubwa na wakisasa ambao hata wao hawana "Tanzania National Stadium"

Ikitokea tukapoteza mechi yetu na Morocco bado nitafurahi na kuwapongeza wachezaji wetu na kuwatia nguvu ili Ivory Coast waje tu kuuwawa mechi ya Nyumbani,tunajenga timu na hapa tulipo si haba.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!