Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 June 2013
Thursday, June 06, 2013

CECAFA



Tamko La CECAFA Kuhusu Timu Kujitoa Kwenye Michuano.

Baraza la soka kwa nchi za Afrika Mashariki na kati CECAFA, limesema linaendelea na matayarisho ya michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati maarufu kama kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi June 18 huko Darfur nchini Sudan.

Katibu Mkuu wa CECAFA Nicolaus Musonye akizungumza  kutokea Nairobi amesema hawana taarifa yeyote ya timu kujitoa katika michuano hiyo na kwamba wao wanaendelea na maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.
 
Kufuatia taarifa kuwa timu ya Tusker ya Kenya imejiondoa katika michuano hiyo ikihofia usalama wao huko Darfur Sudan. Nicolaus" Amesema Tanzania Ni Muhimu sana na hakuna CECAFA Bila Tanzania, Taarifa ya Kuvaa Bullet Proff Sio kweli kwani Nimeenda Sudan na Sikuwa Na Ulinzi wowote, aliyesema kuhusu T Shirt za kuzuia risasi ni muongo"

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!