Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 May 2013
Thursday, May 23, 2013

UDHAMINI WA VILABU VYETU HAPA TANZANIA.


NA JOACHIM SOLOGO 

 Habari wadau wa Blog yetu pendwa ya Soka Stadium. Leo nimeona ni vyema tushirishane mada hii inayohusu udhamini wa vilabu vyetu hapa nchini. Ni muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia udhamini wa vilabu vyetu lakini ninaona kama maigizo. Vilabu vingi vinavyoshiriki ligi kuu hapa nchini havina udhamini huku vile vyenye udhamini ukionekana kutokidhi haja lakin pia ni wa magumashi. Hivi ni nani anayepaswa kulaumiwa ktk jambo hili? Je ni vilabu au makampuni? Au je ni TFF? Bado napata kigugumizi. Hivi ni kweli makampuni ya hapa nchini hayaoni umuhimu wa kujitangaza kupitia vilabu vyetu? Au klabu zetu ni tajiri kiasi kwamba hazihitaji udhamini wa makampuni haya?

 Nilifika mbali zaidi na kujiuliza kama kuna umuhimu wa klabu kuwa na mdhamini au kampuni kujitangaza kupitia club. Hivi ni nani anayefaidika zaidi katika udhamini na kujitangaza, ni kampuni au club? Toka mwaka jana nimeifuatilia kwa ukaribu club ya Simba katika suala la jezi inazovaa, katika jezi za Simba nimeona kuna nembo ya Adidas. Swali la kujiuliza, hivi kweli Simba wanadhaminiwa na adidas? Au wanavaa tu bila kutambua kwamba wanaitangaza Adidas ambayo ni kampuni kubwa sana ya vifaa vya michezo yenye maskani yake huko Marekani.

 Ni wakati wa Watanzania kufumbua macho na kuangalia namna ya kupata wadhamini kwa mikataba inayoeleweka, vilabu vingi Duniani vimekuwa vikinufaika na udhamini wa makampuni tofauti duniani. Ndiyo maana hivi karibuni umeshuhudia Man City wakibadili udhamini kutoka UMBRO kwenda NIKE huku Arsenal nayo ikikamilisha udhamini kutoka NIKE kwenda PUMA. Hayo yote yanatokana na vilabu kuangalia mdhamini anayetoa dau kubwa. Real Madrid nao wameridhia kubadili mdhamini kutoka kampuni ya kamali ya Bwin kwenda Fly Emirates ambayo ni kampuni kubwa ya usafiri wa ndege duniani kote.

 Kwa mtazamo wangu ninaona tatizo kubwa la klabu zetu kukosa udhamini ni uongozi mbovu. Kumekuwa na uongozi mbovu kutoka Shirikisho la Soka hapa nchini (TFF) hadi ktk vilabu. Mnakumbuka sakata la African Lyon kuhusu udhamini wao wa Zantel, TFF walifanya udhamin wa African Lyon kuwa batili kwa sababu ya wao TFF kukurupuka ktk udhamini wao na Vodacom na kujikuta wakiweka kipengele kinachozuia klabu kudhaminiwa na kampuni yenye ushindani na Vodacom.

 Walisahau kuwa siku hizi kipengele hicho kimeondolewa ktk nchi nyingi Duniani, mfano mzuri ni English Premier League maarufu kama Barclays Premier League kutokana na kudhaminiwa na Benki ya Barclays. Pamoja na kwamba Barclays benk ndiyo wadhamini wa ligi kuu ya Uingereza hawazuii club kudhaminiwa na Benk yoyote, mfano mzur ni club ya Liverpool inayodhaminiwa na benki ya Standard Chartered ambayo ni mshindani mkubwa wa Barclays katika huduma za kibenki pale Uingereza na duniani kwa ujumla. Naona sasa umefika muda wa kubadili mfumo wetu wa soka ili tuweze kunufaika na mikataba minono ya makampuni mbalimbali, hii itasaidia kukua kwa soka letu hapa Tanzania

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!