Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 May 2013
Saturday, May 25, 2013

NIONAVYO MIMI TOFAUTI YA FC PORTO VS ARSENAL FC


BY,JOACHIM SOLOGO


Hizi ni timu mbili ambazo miaka ya hivi karibuni zimekuwa na desturi ya kuuza wachezaji wake wengi pengine kwa sababu ya kujenga uchumi wa timu husika. Kwa mfano miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia Arsenal ikiwauza nyota wake muhimu kama vile Samir Nasri, Gael Clichy, Cesc Fabrigas, Alex Song, Robin Van Persie achilia mbali wengineo kama vile Mathiew Flamin, Thiery Henry na Vieira.

 Kwa upande wake Porto imewauza wachezaji kama vile Deco, Hulk, Radamel Falcao, Deco De Souza, Maicon, Bosingwa, Pepe, Anderson, Quaresma, Raul Meireles na wengine wengi.  Lakini pia FC PORTO wamewauza makocha wao kama vile Jose Mournho na Andre Via Boaz. Kwangu mimi naona Arsenal na Porto wamefanana katika sela ya kuuza nyota wao bila kujali umuhimu wao katika timu, lakini FC PORTO wamewazidi Arsenal katika kipengele kimoja muhimu sana. Hiki ni kipengele cha mafanikio. 

Pamoja na kwamba FC Porto wanauza sana wachezaji wao lakini bado wamekuwa wakichukua makombe kama kawaida. Kwa Arsenal hali ni tofauti maana wamekuwa na misimu mingi bila kuchukua kombe lolote. Wanauza wachezaji na hawapati makombe, labda kama kombe la Emirates nalo linaingizwa kwenye record. Swali la kujiuliza ni hili; ni wapi Arsenal wanapokosea? Je falsafa yao wameshindwa kuitumia? Kumbuka kwamba FC PORTO wanarekodi ya kutwaa makombe yote muhimu kama vile UEFA CHAMPIONS LEAGUE NA UEFA EUROPA CUP na hata yale ya nchini kwao Ureno.

I SALUTE YOU FC PORTO” VIVA FC PORTO!!!!!

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!