Kamati ya maandalizi ya michuano ya Kombe la dunia
nchini Qatar mwaka 2022 imetetea Uhalali wa mkataba wake wa kuandaa
michuano ya kombe la dunia baada ya Gazeti moja kudai kuwa lina mashaka
na mchakato wa maandalizi unavyoendelea.
Lakini kamati ya maandalizi ya kombe la dunia nchini Qatar imesema mkataba uliopata ulifuata sheria za Fifa na kuwa haikua ikifahamu shutuma zozote zinazohuzu makubaliano ya kibiashara baina ya watu hao wawili.
Gazeti hilo limedai kuwa Warner na Watoto wake wamelipwa kiasi hicho cha fedha na kampuni inayomilikiwa na Mohamed Bin Hammam.
Bin Hammam alikuwa mtu mwenye nguvu kubwa ndani ya Fifa kwa miaka mingi lakini alipewa adhabu ya kufungiwa maisha kushiriki maswala yahusuyo shirikisho hilo baada ya kushutumiwa kuwa na maslahi binafsi alipokuwa Kiongozi wa shirikisho la soka barani Asia.
Nyaraka ambazo gazeti la Telegraph limedai kuziona, huenda zikazua maswali mengi kutoka kwa Mkuu wa uchunguzi wa maswala ya maadili ndani ya Fifa, Michael Garcia, ambaye anachunguza namna gani ambavyo haki za maandalizi ya michuano hiyo zilipatikana kwa ajili ya mwaka 2018 na 2022.
katika taarifa yao, Waandaaji wa michuano hiyo nchini Qatar wamesema haki ya kuandaa michuano hiyo ilifuata taratibu zote za Fifa na kufuata maadili yote.
Warner na Bin Hammam walikataa kutoa kauli juu ya madai yaliyotolewa dhidi yao walipoulizwa na BBC kuhusu tuhuma kutoka gazeti la the Daily Telegraph.
0 comments:
Post a Comment