Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 March 2014
Saturday, March 22, 2014

PAUL SCHOLES ASEMA HAKUNA ANAYEJUA HATIMA YA UNITED



Mkongwe wa klabu ya Manchester United Paul Scholes, siku ya Jumamosi ya leo ameibuka na kuungwa mkono pale aliposema kuwa,United wanamatumaini makubwa ya  kuwapiga Bayern Munich na kwenda moja kwa moja fainali ya Ligi ya Mabingwa - hata bila ya  Robin van Persie mshambuliaji wao ambaye amepata majeraha na atakosa mechi hiyo na nyingine nyingi za EPL.
Scholes alikiri match yao classic ya mwaka 1999 , ambayo yeye aliikosa kupitia kutumikia adhabu yake ya kusimamishwa,United walifanikiwa kushinda dakika za majeruhu kwa mabao 2-1, amesema mechi hiyo ya kihistoria,isichukuliwe kama kipaumbele cha kwanza kwa meneja David Moyes.
Lakini kiungo huyo mstaafu, 39, akizungumza wakati akiwa safarini huko Singapore , amekuwa na matumaini kuhusu nafasi ya United kwenda nusu fainali huku akisema kuwa "kwa kucheza mechi mbili, tunaweza kumpiga mtu yeyote ."
"Moja ya timu ambazo pengine hakuna ambaye angependa kukutana nayo ni Bayern Munich lakini kama tunaweza kuwapiga ,nani ambaye anajua, tunaweza kwenda mpaka fainali ," Scholes aliwaambia waandishi wa habari .
Mabingwa wa Uiingereza, kwa sasa wanashika nafasi ya saba katika Ligi Kuu, wanatakiwa kukabiliana na na timu ya Pep Guardiola ya Bayern , ambayo iko juu ya msimamo wa Bundesliga katika muda huu na kuna uwezekano wa kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa huo mapema mwishoni mwa mwezi huu.


Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Robin van Persie ameripotiwa kwamba amepata majeruhi ya goti baada ya kuumia katika mchezo wa raundi ya pili wa hatua ya 16 ya ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Olympiakos uliopigwa katika dimba la Old Trafford, jumatano wiki hii.

Van Persie ambaye alifunga hat trick iliyoipeleka Man United hatua ya robo fainali alitolewa nje na machela katika mchezo huo katika dakika za mwisho za huo, na leo hii baada ya kufanyiwa vipimo kiundani imegundulika amepata majeruhi yatakayomuweka nje kwa muda wa wiki 4-6.


Kwa maana hiyo mdachi huyo ataukosa mchezo dhidi ya Manchester City pamoja na mchezo wa kwanza wa robo fainali ya UCL dhidi ya Bayern Munich, hivyo kuiachia timu yake pigo zito.



0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!