Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 March 2014
Friday, March 21, 2014

MECHI YA 1,000 KWA WENGER MIKONONI MWA MOURINHO.



Arsene Wenger anategemea kusherehekea mechi yake ya 1,000 kama mwalimu wa Arsenal kwa kupunguza mwanya kati ya klabu yake na Chelsea katika uongozi wa ligi ya Premier ya Uingereza wakati atakapotewambeza vijana wake kukabiliana na waasimu wao wa jiji la London Jumamosi. 

Wenger ameshikilia hatamu ya uongozi Arsenal kwa miaka 18 sasa na ukame wa taji la Premier kwa mika tisa sasa lakini ushindi wao ugenini dhidi ya majirani wao Tottenham juma lililopita uliongezea matumaini baada ya Chelsea kubwagwa 1-0 na Aston Villa. 

Huku wakiwa na mechi moja ya ziada dhidi ya Chelsea, Wenger ana kibarua kigumu cha kumlaza mwalimu mwenzake Jose Mourinho kwa mara ya kwanza katika majaribio kumi ili kupata faida katika harakati za kuwania taji hilo. 

Arsenal pia wamefuzu semi fainali za kombe la FA na Wenger amekiri hali wanayoipata kwa sasa,imezua kumbu kumbu za enzi ambayo klabu yake iliweza kushinda vikombe mara kwa mara.
“Muda huo wote ulienda wapi? Inaonekaa kama nilianza hapa juzi tu! Siamini imekuwa kipindi kirefu kiasi hicho,” Wenger aliambia tovuti rasmi ya Arsenal. 

“Kinacho saidia ni kuongeza umakini kwenye kila mechi inayofuata na ukitizama nyuma, ninafikiria kuwa nimedumu kipindi kirefu hapa na nitaendelea kujaribu kuimarika kila mara,” aliongeza. 

“Mechi dhidi ya Arsenal inakuja muda bora kwani tulishindwa mechi iliotangulia. Tumepumzika kwa usaidizi wa wafanyi kazi wa hapa na tunalenga kutia bidii mbele ya mashabiki wetu,” nyota wa Chelsea, Eden Hazard, kwa upande mwingine, aliambia tovuti la timu yake.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!