FIKIRIA
kuwachezesha Cristiano Ronaldo na Robin van Persie kwenye safu ya
ushambuliaji ya timu yako dhidi ya timu ambayo Neymar na Lionel Messi
wanaongoza mashambulizi yake?
Unapozungumzia fantasy football (Soka la ndoto)…. hili ndiyo kiboko yao.
Kampuni
ya Fans All Star Football (FAS) inawapa nafasi mashabiki wa soka
duniani kote kuchagua kikosi chao cha wakipendacho kutoka kwa wachezaji
bora Ulaya na duniani kwa ujumla.
Baada
ya upigaji kura kumalizika mashabiki wa soka watapata nafasi ya
kushiriki shindano la kupambana na timu iliyochaguliwa na wataalamu wa
soka na kushindani kiasi cha pauni milioni 50,000.
Supa Staa: Mshambualiaji wa Real Madrid, Mreno Cristiano Ronaldo yupo kwenye orodha ya nyota wa Ulaya
Cristiano Ronaldo akionyesha mwili wake uliojengeka akiwa Miami (picha ndogo) katuni Johnny Bravo
Kuepusha
zoezi hilo kuwa gumu, mfumo unatumika ni 4-4-2. Fikiria Ronaldo,
Gareth Bale, Andrea Pirlo na David Beckham kwenye timu moja? Van Persie
atatengenezewa nafasi kibao. Hiyo inaweza kuwatisha mabeki lakini ni
bonge la burudani kwa mashabiki.
Tofauti
na kura za Fans All Star Global, wale watakaoshiriki watapata nafasi ya
kuonyesha uwezo wao kwenye soka kwa kupambana na magwiji kwenye
Shindano la FAS.
Mashabiki
watapata nafasi ya kushinda kiasi cha pauni 50,000 kama wakifanikiwa
kutengeneza kikosi kama kile ambacho kitatengenezwa na wataalamu wa Fans
All Star ambao ni Kocha wa zamani wa England, Glenn Hoddle na
Muargentina Bingwa wa Kombe la Dunia, Ossie Ardiles.
Viwango vya dunia: Robin van Persie na Gareth Bale ni miongoni mwa nyota wa Ligi Kuu England
Wawili: Mkali wa mabao wa Barcelona, Lionel Messi na mchezaji mwenzake mpya, Neymar wanaongoza vipaji vingine duniani
Zawadi: Watumiaji wa Fans All Star wanaruhusiwa kuchagua timu na kupambana na timu ya wataalamu kuwania pauni 50,000
Chagua timu yako ya FAS
Ilikufanikiwa katika hili mashabiki watatakiwa kununua ‘bundles’ za Kura na kuingiza vikosi vya ziada.
Washiriki
wa Fans All Star wataweza kuchagua kikosi cha wachezaji 15 cha kikosi
cha Ulaya na kile cha kikosi cha Ulimwengu mzima (Wachezaji 11 wa kuanza
na wanne wa benchi) wachezaji hao watakuwa kati ya wachezaji bora 1100,
550 watakuwa wa Ulaya na 550 wengine watakuwa wa Ulimwengu wote.
Jumatatu
ijayo idadi ya kwanza ya wachezaji 1100 itapunguzwa kufiki 660 kutokana
na kura za mashabiki, idadi hii itapunguzwa tena Alhamisi ya Agosti 1
na kubaki 110, upigaji kura utafika tamati Agosti 31 mwaka huu.
Kikosi cha kwanza cha wataalamu wa Fans All Star kitatangazwa Jumanne ya Septemba 1 mwaka huu.
Kuchagua timu yako Ulaya na Ile ya Dunia unatakiwa kuingia kwenye mtandao wa www.fansallstar.com
0 comments:
Post a Comment