BEKI wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa amesema klabu hiyo
imefanya usajili mzuri mpaka sasa, licha ya kubezwa na baadhi ya wadau
lakini amemkingia kifua kipa wa heshima Msimbazi, Juma Kaseja.
“Wengi wanaona kama Simba imefanya usajili wa
kiwango cha chini eti kwa sababu ina wachezaji wengi vijana na wana
wasiwasi kuwa timu inaweza kufanya vibaya msimu ujao ila mimi nawaunga
mkono kwa usajili waliofanya na utawabeba,”alisema Pawasa na kushauri
Simba itafute beki wa kati.
“Ukiangalia kitu kikubwa kilichoigharimu Simba
msimu uliopita hasa hasa ni safu ya ulinzi na hiyo ndiyo inatakiwa
kwenye usajili huu ipewe kipaumbele, kwani muda mwingine unaweza
ukamlaumu tu kipa Juma Kaseja kumbe safu ya ulinzi imemgharimu. Lazima
uangalie muda mwingine kipa anakuwa bora kutokana na uwezo wake au
anabebwa na mabeki wake bora, sasa safu ya ulinzi ya Simba haikuwa bora
msimu uliopita hivyo hata kipa hataonekana bora.
“Naamini Kaseja ni kipa mzuri na ana uwezo, hayo
yote yanayotokea ni upepo tu, haitajiki kuvunjwa moyo kama watu
wanavyofanya sasa, yule ni kipa wa timu ya Taifa lazima apewe heshima
yake na isitoshe kaichezea Simba muda mrefu na naamini bado ana uwezo wa
kucheza kwa kiwango kwa muda mrefu,”
alisema Pawasa ambaye ni miongoni mwa wachezaji wa zamani wenye taaluma. Simba inadai imemwambia Kaseja aamue anataka kusajiliwa kwa mkataba wa aina gani.
alisema Pawasa ambaye ni miongoni mwa wachezaji wa zamani wenye taaluma. Simba inadai imemwambia Kaseja aamue anataka kusajiliwa kwa mkataba wa aina gani.
0 comments:
Post a Comment