Searching...
Image and video hosting by TinyPic
29 January 2017
Sunday, January 29, 2017

BARCELONA YAVUTWA SHATI, SEVILLA HOI



Na FLORENCE GR

Mabingwa wa soka wa nchini Hispania klabu ya Fc Barcelona kwa mara nyingine tena wamevutwa shati mara baada ya kutoa sare ya goli 1-1 dhidi ya Real Betis na kufanya tofauti ya pointi baina nao na viongozi wa ligi hiyo klabu ya Real Madrid kufikia pointi moja huku wakiwa na michezo miwili mkononi .

Klabu hiyo ikiongozwa na nyota wao watatu maarufu kwa jina la MSN ilijikuta ikibanwa kila idara na wenyeji wao hivyo hadi kipindi cha kwanza kinaisha timu hizo hazikuweza kufungana ,kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Barcelona walijikuta wakiuhusu bao kunako dakika ya 75 goli lililofungwa na Alegria Moreno.

Hata hivyo goli la Alex Vidal halikukubaliwa na mwamuzi mara moja lakini baada ya picha za video kurudiwa ilionekana mpira ulikuwa umeshavuka mstari na Barca walilazimika kusubiri hadi dakika ya 90 pale nyota wa Uruguary Luis Suarez alipoisawazishia timu hiyo akipokea pasi nzuri kutoka kwa Lionel Messi hivyo kuifanya timu yake kutoondoka mikono mitupu katika mchezo huo.

Katika ligi tano bora barani ulaya La Liga tu ndo ligi ambayo haitumii 'Goal Line Technology' ambapo inatumika katika ligi kuu nchini Uingereza, Ufaransa, Italy na Ujerumani.

Viongozi wa soka nchini Hispania wameendelea kusema kuwa hawataweza kutumia mfumo huo kwani ni ghali sana lakini kukataliwa kwa goli la Barcelona kunasadikiwa  kutaongeza jitihada za mfumo huo kutumika katika ligi hiyo.

Baada ya mchezo huo kocha wa Bacelona Luis Enrique alionekana kujibu kidiplomasia zaidi pale alipoulizwa kuhusu tukio la kunyinywa goli kwa timu yake akisema kuwa 'waamuzi wanaihitaji msaada iwe kamera au vyovyote'

Sasa Barcelona imeshuka dimbani mara 20 na  inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 42 sawa na Sevilla huku ikiwa na idadi kubwa ya magoli ya kufunga na kufungwa  huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Real Madrid ikiwa na pointi 43 ikishuka dimbani mara 18.

Katika mchezo mwingine imeshuhudiwa vijana wa Jorge Sampaoli timu ya Sevilla kungwa mabao 3-1 dhidi ya Espanyol ambao ni wapinzani wa Fc Barcelona hivyo kuwashuka hadi nafasi ya tatu na pointi zao 42.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!