Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 April 2015
Wednesday, April 08, 2015

ZAKHEM FC /FFU SC, KUSAKA BINGWA WA JUMLA MICHUANO YA LIGI YA MKOA DAR ES SALAAM.


 


Baada ya kumalizika kwa michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam na kupata timu tatu zitakazouwakilisha mkoa katika michuano ya ligi ya mabingwa ya mikoa ya TFF,kesho Alhamis Aprili 09/2015,katika uwanja wa Karume jijini kutakuwa na mchezo wa fainali ya kumpata Bingwa wa jumla wa michuano ya ligi ya mkoa.

Timu zitakazoumana katika fainali hiyo ni ZAKHEM FC dhidi ya FFU SC,ambazo zitashuka dimbani majira ya saa kumi jioni zikishuhudiwa na umati wa mashabiki waliokuwa wakiyafuatilia mashindano hayo tangu yalipoanza kutimua vumbi.

Kwa mujibu wa kamati ya mashindano ya chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,timu zilizofanikiwa kuuwakilisha mkoa katika michuano ya ligi ya maabingwa ni pamoja na ZAKHEM FC,FFU SC na CHANGANYIKENI SC.
Mwenyekiti wa DRFA,Almas Kasongo,ameipongeza kamati hiyo ya mashindano kwa kusimamia vizuri uendeshaji wa ligi tangu ilipoanza.
 
Imetolewa na DRFA,
Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano DRFA
Omary Katanga/+255766358585/+255784500028
 

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!