Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 April 2015
Thursday, April 16, 2015

Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ni "Balaa"


Na George Mganga
Ulimwengu wa soka kwa miaka ya karibuni umetawaliwa na wachezaji wawili, mmoja wa FC Barcelona na mwingine ni mkali toka kikosi cha Real Madrid .
Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kwa pamoja wamekuwa katika kiwango ambacho kimewafanya waonekane kama watu wanaotoka kwenye sayari nyingine hali ambayo imezua upinzani kati yao.. story zao huwa hazikauki na kwenye HEADLINES za michezo, hata vijiweni pia.
Moja ya hoja ambazo zimekuwa zikiibuka ni nani kati ya wawili hawa ni bora kuliko mwingine, hoja hii imezaa swali jingine miongoni mwa watu ya kwamba ingekuaje kama wachezaji hawa wangekuwa kwenye timu moja??
Ni vigumu kwa hili kutokea kwani kwa sasa wanacheza kwenye timu zenye utamaduni wa upinzani na wanakoelekea ni vigumu kuona wakibadilishana timu siku moja yaani eti kumuona Ronaldo akichezea Barcelona na Messi akichezea Madrid ??
Sio hapo tu.. hata kwenye timu ya taifa uwezekano huo haupo kwani Messi ni Muargentina na Ronaldo anatoka Ureno.
Jarida la Mundo Deportivo limeripoti mpango wa kuandaa mchezo maalum wa wachezaji nyota barani ulaya .
Hata hivyo ndoto ya wawili hawa kuonekana wakichezea timu moja huenda ikawa kweli baada ya jarida moja la Hispania Mundo Deportivo kuripoti mpango wa kuandaa mchezo wa wachezaji nyota toka klabu mbalimbali barani ulaya.
Hii imetokana na wazo kama la mchezo wa Ligi ya Basketball Marekani NBA, yaani NBA All Star ambapo wachezaji huchaguliwa na kuwakilisha kambi za mashariki na magharibi na kwa Ulaya zitachaguliwa timu mbili zikiwakilisha wachezaji toka vilabu vya Ulaya Kaskazini na Kusini.

Wazo hili litahusisha wachezaji watakaochaguliwa na mashabiki kupitia mtandao ambapo kutakuwa na wastani wa wachezaji watatu toka klabu moja na hapa ndio uwezekano wa kuwaona Messi na Ronaldo wakiwakilisha Hispania ambayo iko kwenye eneo la kusini mwa Ulaya.
Wachezaji wengine nyota kama Zlatan Ibrahimovic , Gareth Bale, Neymar na Edinason Cavanni pia wanaweza kujumuishwa kwenye kikosi cha Ulaya Kusini ambacho kitakuwa na klabu za mataifa kutoka Ureno, Hispania na Ufaransa.
Wachezaji kama Wayne Rooney, Angel Dim Maria, Sergio Aguerro , Alexis Sanchez na Edin Hazard pamoja na wachezaji nyota wa Bayern Munich watawakilisha kikosi cha klabu za Ulaya Kaskazini.
Hata hivyo bado wazo hili halijawa rasmi na haijafahamika kama litafanyiwa kazi kikamilifu na kuweza kutimiza azma ya mashabiki ya kuona mkusanyiko wa wachezaji nyota wakiwa wanacheza kwenye timu moja.
Story ni kwa mujibu wa Millard Ayo

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!