Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 February 2015
Monday, February 23, 2015

Azam safarini hapo kesho.


Na Oscar Oscar Jr

Baada ya kutoka sare mara mbili mfululizo kwenye ligi kuu ya Vodacom, mabingwa watetezi timu ya Azam imepoteza Uongozi wa ligi kuu na sasa ligi hiyo inaongozwa na mabingwa mara 24 timu ya Yanga. 

Yanga kwa sasa wametimiza alama 31, Azam wakibakia na alama 27 huku nafasi ya tatu ikikamatwa na Kagera Sugar ambao wana pointi 24 wakiwa na mchezo mmoja zaidi.

Matajiri hao wa Jiji la Dar es Salaam, wanajiandaa hapo kesho kuanza safari yao kuelekea nchini Sudani ambako watakwenda kupambana na El-Merreikh ya Sudani kwenye mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika ambapo mchezo wa awali uliopigwa nchini Tanzania, Azam waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mchezo huo wa marejeano unatarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili majira ya saa mbili usiku. Akizungumza na E-Sports ya EFM, Msemaji wa wana lambalamba hao, Jaffari Idd Maganga amesema kuwa hali za wachezaji na nzuri na kikosi kizima nchini Sudani hata wale ambao hawatocheza mchezo huo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!