Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 January 2015
Thursday, January 01, 2015

Uchambuzi: Manchester City vs Sunderland


Na Chikoti Cico

Katika mfululizo wa mechi za ligi kuu nchini Uingereza kwa mzunguko wa pili, kwenye uwanja wa Etihad timu ya Manchester City itaikaribisha Sunderland katika mchezo ambao kila timu inahitaji ushindi na kuweza kuanza vyema mwaka mpya wa 2015.

Manchester City baada ya kutoka sare ya magoli 2-2 kwenye mchezo uliopita dhidi ya Burnley na hivyo kupoteza nafasi ya kuikaribia Chelsea kwenye msimamo wa ligi na kuendelea kushika nafasi ya pili ikiwa na alama 43.

Timu hiyo inatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo kwa nguvu ila kupata ushindi na kuifikia Chelsea ambao imejikusanyia alama 46.

Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini kwenye mchezo huo atawakosa Vicent Kompany, Edin Dzeko na Sergio Aguero ambao ni majeruhi huku Frank Lampard akiruhusiwa na timu yake ya New York City kuichezea Man City dhidi ya Sunderland.

Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha kiungo wa Manchester City James Milner amefunga magoli mengi dhidi ya Sunderland kuliko timu nyingine yoyote, amefunga jumla ya magoli matano.

Kikosi cha Manchester City kinaweza kuwa hivi: Hart, Zabaleta, Demichelis, Mangala, Clichy; Fernandinho, Toure; Nasri, Silva, Milner; Jovetic

Sunderland ambao walitoka sare ya 0-0 dhidi ya Aston Villa kwenye mchezo uliopita na kupata alama moja muhimu hivyo kushika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 20 wanatajiwa kucheza kwa ari na nguvu ili kushinda mchezo huo.

Kocha wa Sunderland Gus Poyet kwenye mchezo huo atawakosa Liam Bridcutt, Patrick van Aaholt na Anthony Reveillere ambao ni majeruhi huku kiungo Sebastian Larsson ambaye aliumia kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa akiwa na hatihati ya kucheza dhidi ya City.

Takwimu zinaonyesha Sunderland wamekuwa na matokeo mabovu kwenye uwanja Etihad kwani katika michezo 10 iliyopita ya ligi wamefungwa michezo nane na kutoka sare michezo miwili bila ya kushinda mchezo wowote huku pia wakiruhusu nyavu zao kutikiswa mara 28 na Manchester City.

Kikosi cha Sunderland kinaweza kuwa hivi: Pantilimon; Vergini, O'Shea, Brown, Jones; Cattermole, Larsson, Rodwell; Giaccherini, Johnson; Wickham

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!