Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 January 2015
Saturday, January 03, 2015

MSUVA KAANDAE SHAMBA MAPEMA


Na Peter Richard Kabita 
0765178880 

Kipindi cha mvua ndio hichi kama wewe ni mkulima wa kweli ndio kipindi cha kuandaa mashamba kwa kilimo. ni kweli tuandae mashamba na tupande mapema hali ya hewa haiaminiki, ukichelewa mvua ikikata imekula kwako.

Leo nilikuwa nataka kumkumbusha ndugu yangu, kiungo mshambuliaji wa Yanga Simoni Msuva. Huu ndio msimu wa mvua, andaa shamba mapema mvua ikikata mzao yatagoma kuota.

Najua kwa sasa upo kwenye klub nzuri zenye kukupa kipato kikubwa kwa hapa nchini. Usizubae na milion moja, mbili au tatu japo sizani kama inafika unazopewa kwa mwezi hapo ulipo. 

Nenda shamba tafuta timu nje kwa kiwango chako na umri wako naamini unaweza kucheza soka popote pale duniani sio lazima uende Ulaya moja kwa moja, kina Obi Mikel walizunguka kwingine kabla kabla ya kutua EPL.

Mbwana Samatta ni moja kati wachezaji wanaolipwa vizuri na yupo tu hapo Dr Congo akikipiga na TP Mazembe. Unadhani angebakia Simba hali ingekuwaje? Yuko wapi Mrisho Khalfani Ngassa? taratibu ameanza kupotea.

Hapa bongo utaishia kupata sifa tu mwisho wa siku tutakusahau. Mpira wa bongo ni kama mvua, inaweza kunyesha muda mfupi kisha ikapotea kabisa.

Ukiendelea kulewa sifa, utaambulia kununuliwa Gari na biashara itakuwa imekwisha. Hakuna kitu kinachowapumbaza wachezaji wa kitanzania kama kununuliwa Gari. Hivi kwa nini msiwe mnapewa hela kisha Gari mkanunua wenyewe?

Ngassa kutoka Azam kwenda Simba, tuliona akipewa Gari. Wakati Mkude anataka kuondoka Simba msimu huu, tukaona anatulizwa kwa kupewa gari na baadaye akasaini mkataba wa kubaki msimbazi. Tatizo ni gari?

Mwinyi Kazimoto huenda akawa anacheza kwenye ligi ambayo sio bora sana kule Qatar lakini ni rahisi kwake kusonga mbele kuliko kuendelea kubaki hapa nyumbani. Anakutana na watu wengi, anakumbana na changamoto nyingi za kumsogeza mbele.

Hawa kina Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta hawana mpango tena wa kuziwaza Simba na Yanga, hawana mpango za Azam wala Mbeya City. Wanafikiria ni lini watacheza ligi nchini Ufaransa, ni lini watakwenda Hispania kujiunga na ligi ya segunda (Ligi daraja la pili-Hispania).

Mchezo wa soka ni tofauti na Filamu, soka ni tofauti na muziki ambapo hata ukiwa na miaka 70, unauwezo wa kutoa "singe"  au filamu moja na ukauteka ulimwengu. Simnakumbuka Bibi Cheka? ghafla amekuwa mwanamuziki ukubwani na maisha yameendelea. Ukicheza na muda, kwenye soka utabaki na stori tu.

Ni vigumu sana kwa mwanasoka kubaki kwenye ubora wa juu kwa zaidi ya miaka 10. Hata kina Frank Lampard na Steven Gerrard, waliwahi kuwa vijana lakini kwa sasa ubora umepungua. Nguvu za miguu zimepungua na hata pumzi imekata.

Ni vema kuutumia muda huu wa ujana, kutengeneza mwelekeo ambao utakufanya uishi maisha mazuri hata kama umestaafu soka. Msuva kama utaendelea kubaki hapa nchini, maisha ya soka yatakuwa na muda mfupi sana kwake hasa ukizingatia kuwa timu zetu zinaongozwa na viongozi wasio ijua kesho.      

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!