Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 January 2015
Saturday, January 03, 2015

Kumbe Wenger bado hajaacha mambo yake.


 Na Oscar Oscar Jr

Katika hali ambayo inaashiria kutobadilika kwa Kocha wa Arsenal, mzee Arsene Wenger badala ya kuwania wachezaji wenye majina makubwa na walio tayari kupambana kutokana na msukumo kutoka kwa mashabiki, yeye yuko mbioni kumnasa kiungo wa Ipswich, Teddy Bishop 18 kwa ada ya Pauni 10M.

Kiungo huyo atamlazimu Wenger kupambana vilivyo kwani ana waniwa pia na klabu ya Manchester United. Hii ni habari ambayo haiwezi kuwapendeza mashabiki wa Arsenal ambao wanaonekana kukataa tamaa ya kupata tena mafanikio wakiwa na kocha huo raia wa Ufaransa.

Kwa upande wa pili, Gunners na Liverpool wameonekana pia kupigana vikumbo kuwania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Lazio, Keita Balde Dia. 

Mshambuliaji huyo 19, anatajwa kuwa na thamani ya Pauni 15 M na klabu ya Lazio inaonekana kuwa tayari kufanya mazungumzo na klabu inayomuhitaji. 

Arsenal ambao wametoka kupoteza mchezo wao wa ligi kuu mbele ya Southampton kwa mabao 2-0, wanaonekana kuwa na uhitaji wa kiungo mkabaji, beki wa kati na mshambuliaji mmoja mwenye uwezo mkubwa ili aje kusaidiana na Alexies Sanchez ambaye mpaka sasa amefunga mabao 10.

Pengine kwenye taarifa za muda huu ambazo arsenal wanaweza kufurahia ni timu yao kuhusishwa na usajili wa kiungo wa Borussia Dortmund,  Ilkay Gundogan ingawa Liverpool nao wameonekana kumuhitaji. 

Kiungo huyo mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2016 na anaonekana kukataa kuongeza mkataba mwingine hivyo inaweza kuwa fursa nzuri kwa timu inayomuhitaji.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!