Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 January 2015
Sunday, January 04, 2015

KUELEKEA MECHI YA AZAM vs KMKM





  Na Peter Richard Kabita- 0765 178880  

Jioni ya leo zinakutana timu bingwa kutoka kila upande Azam ni bingwa mtetezi tanzania bara huku Kmkm akiwa bingwa mtetezi wa tanzania visiwani. 

 Hii itakuwa mechi yao ya pili kukutana baada ya kukutana mara ya kwanza kwenye mashindano ya klabu bingwa afrika mashariki maarufu kama kagame ambapo mpira ulimalizika kwa suruhu ya bila kufungama.
 Kmkm inaingia kwenye mechi hii ngumu huku ikiwa na rekodi ambayo sio nzuri sana kiwango chao cha sasa sio kama kile cha zamani hata kwenye msimamo wa ligi kuu Zanzibar inakamata nafasi ya nane ikizipita timu nne tu nyuma.

Japo ilidroo kwenye mechi yao na Mtende kwenye mashindano haya ya mapinduzi bado wanakazi ngumu kukabiliana na wanalambalamba hao huku kocha mkuu wa Kmkm Shaban Ramadhan tangu aondoke kocha Ally Bashiri amekuwa na matokeo yakutoridhisha kabisa .


Azam Fc inaingia uwanjani bila ya wachezaji wake wengi tegemeo kwa sababu tofauti ikiwemo majeruhi itawakosa, Aishi Manula, Gardiel Michael, beki Pascal Wawa, mapacha Kipre Tcheche na Bolou  pamoja na mshambuliaji wao aliyekuwa na wastani mzuri wa kufunga kwa mechi za karibuni Didier Kavumbagu naye hato kuwepo. 

Japo Azam inakikosi kipana kukosekana kwa wachezaji wao hawa itakiwa tatizo kwa kiasi flani nategemea kumuona Amri Kiemba akianza leo kwenye safu ya ushambuliaji John Boko atasimama mbele pamoja na matokeo ya nyuma ya Azam sio mazuri sana kwani katika mechi tano za mwisho walizocheza Azam kuanzia za kirafiki kule Uganda hadi mechi yao ya mwisho ya kombe la mapunzi dhidi ya Kcca walikuwa wamecheza mechi tano huku wakiwa wameshinda mechi moja tu waliyoifunga Vaipers 3-1.

 Wamefungwa mechi mbili na kutoka sare mechi mbili uku kwenye msimamo wa ligi ikiwa nafasi ya tatu nyuma Mtibwa na Yanga. Pamoja ma kutokuwa na matokeo mazuri bado Azam inanafasi kubwa kuelekea mechi ya leo, kwanza vipaji vya mchezaji mmoja mmoja, benchi la ufundi ila inatakiwa kuwa makini na mshambuliaji Kambi wa Kmkm japo matokeo ni dakika 90 tusubiri tuone.



0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!