Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 January 2015
Tuesday, January 13, 2015

Bayern Munich haipitiki Ulaya.


Na Chikoti Cico

Klabu ya Bayern Munich inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga imeonekana kuwa na beki bora isiyofungika kirahisi katika takwimu za mwaka 2014-2015 zilizotolewa na Huawei.

Bayern Munich ambayo inaongoza kwenye msimamo wa ligi ya Bundesliga wakiwa na alama 45 wamefungwa magoli manne tu katika michezo 17 ya ligi hiyo ikiwa ni wastani wa 0.24 kwa kila mechi huku kipa wao mahiri Manuel Neuer akizuia nyavu zake kutikiswa (clean sheet) katika michezo 13.

Pia takwimu hizo zinaonyesha timu za  Jevuntus na Barcelona nao wana beki imara kwani katika michezo 18 wamefungwa magoli tisa kila mmoja ikiwa ni wastani wa 0.50 kwa kila mechi huku Juventus wakizuia nyavu zao kutikiswa mara 10 na Barcelona mara 11.

Timu zingine ambazo pia zinaonekana kuwa na beki nzuri ni Saint-Etienne inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1 ambayo ina wastani wa 0.65 kwa kila mechi huku Southampton inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza ikiwa na wastani wa 0.71 kwa kila mechi.

Nao Roma wanashika nafasi ya sita wakiwa na wastani wa 0.72 katika kufungwa magoli huku Valencia wakiwa wamefungwa magoli yenye wastani wa 0.83.

Pia timu za Olympique Lyon, Paris Saint-Germain, Nantes na Lille zote kutoka Ufaransa zinakamilisha timu 10 bora zenye ulinzi bora zikiwa na wastani wa kufungwa magoli 0.85 kwa kila mechi.

Werder Bremen inayoshiriki ligi ya Bundesliga ndiyo timu yenye beki mbovu kati ya timu zote toka ligi tano kubwa barani Ulaya kwani wamefungwa jumla ya magoli 39 katika michezo 17 na kuwa na wastani wa 2.39.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!