Searching...
Image and video hosting by TinyPic
31 December 2014
Wednesday, December 31, 2014

John Bocco na nyendo za Mohamed Hussein "Mmachinga "


Na Samuel Samuel 
0752415551

Miongoni mwa wachezaji ambao wamedumu na timu ya Azam FC toka ilipoingia kwenye soka la ushindani mwaka 2007 ni John Bocco " Adebayor" Ukimwondoa Nadir Haroub wa Yanga ambaye naye amedumu kama timu kapteni, basi John Bocco naye ni mmoja wa makapteni nguli kwa sasa VPL. 

Mchezaji huyo mrefu mwenye nguvu na ustadi mkubwa wa kupachika mabao , amedumu kama tegemeo la Azam FC kwa muda sana. Kinachomfanya azidi kuonekana lulu ni nidhamu aliyonayo, uwezo wa kuwaunganisha wenzake na ufundi wa kupachika magoli muhimu katika nafasi adimu. 

 Juzi mechi na YANGA aliwashitua sana wadau wa soka kwa goli lake. Ilimchukua dk 3 tu toka alipoingia uwanjani na kufunga goli zuri ambalo lilimeacha msiba mzito kwa wana Jangwani. 

Ni aina ya magoli ambayo mshambuliaji huyo wa Azam FC amekuwa akiyafunga lakini goli lile lilitonesha vidonda vya wana Yanga wakiwa na kumbukumbu ya mchezaji huyo huyo kuzima ndoto za ubingwa za Yanga msimu wa 2013-14. 

Azam FC ikishinda 2-1 dhidi ya Mbeya City ni kapteni huyo alisababisha uwanja wa Shekh Amri Abeid Arusha ilipokuwa ikicheza Yanga na Oljoro JKT huku Yanga ikiwa mbele kwa magoli mawili . 

Mashabiki na viongozi walikuwa wanaomba droo ili kufufua matumaini ya kulisaka kombe hilo lakini John Bocco alitupia bao la pili na kuwapa Ubingwa wana lamba lamba hao. 

Mmachinga alidumu kwa zaidi ya miaka 10 akiitumikia Yanga kwa mafanikio makubwa na ameacha mtihani mkubwa kwa mafowadi wa nchi hii baada ya rekodi yake ya magoli 26 kwa msimu mmoja wa ligi haijavunjwa mpaka sasa. Rekodi hiyo imewekwa mwaka 1999. 

Hapo utaona John Bocco  ambaye ni mfungaji bora wa Azam wa muda wote, naye amedumu Azam Fc kwa muda mrefu na bado ana kasi ya kupachika mabao. Katoka katika majeruhi lakini bado ni moto wa kuotea mbali. Mabeki wa ligi kuu wajipange kumzuia mkongwe huyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!