Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 November 2014
Saturday, November 08, 2014

Uchambuzi: Queens Park Rangers vs Manchester City


Na Chikoti Cico

Mchakamchaka wa ligi kuu nchini Uingereza unatarajiwa kuendelea tena kwenye viwanja mbalimbali wikendi hii, kwenye wa uwanja wa Loftus Road timu ya QPR itaikaribisha Mancester City huku kila timu ikihitaji ushindi na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya msimamo wa ligi.

Kocha wa QPR, Harry Redknapp bado ana kibarua kigumu kwani mpaka sasa timu yake inashika nafasi ya 19 ikiwa na alama 7 huku wakiwa wameshinda michezo miwili tu kati ya michezo 10 waliyocheza ya ligi.

Timu ya QPR itawakosa Alejandro Faurlin aliyeko majeruhi huku beki Rio Ferdinand akitumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu kwa matumizi mabaya ya mtandao wa twitter.

Wachezaji wa zamani wa City Joey Barton na Nedum Onuoha ambao walikuwa majeruhi, wanaweza kurejea kuikabili timu yao ya zamani.

Kikosi cha QPR kinaweza kuwa hivi: Green; Isla, Caulker, Dunne, Yun; Fer, Sandro, Henry, Vargas; Zamora, Austin

Manchester City wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na mlolongo wa matokeo mabovu kwani mpaka sasa wamepoteza michezo mitano katika mashindano yote waliyocheza karibuni huku wakiwa na hatihati ya kutokuvuka kwenye hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini anatarajia kuingia kwenye mchezo huo kutafuta alama tatu muhimu lakini zaidi kurudisha ari na hamasa kwa wachezaji wake, kocha huyo atamkosa nahodha Vicent Kompany aliyeumia kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya CSKA Moscow.

Atawakosa Kiungo David Silva na beki Aleksandar Kolarov ambao ni majeruhi, ingawa kiungi Frank Lampard amepona ila anatarajiwa kutokuanza kwenye mchezo huo.

Manchester City ambao wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi huku wakiwa na alama 20 kati ya mechi 10 walizocheza wanaonekana kuwa na takwimu nzuri dhidi ya QPR kwenye mashindano yote waliyokutana kwani katika mechi tano zilizopita City ameshinda michezo minne na kutoka sare mchezo mmoja dhidi ya QPR.

Mshambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko amefunga magoli katika mechi tatu kati ya nne alizocheza dhidi ya QPR wakati huo huo safu ya ushambuliaji ya City inatarajiwa kuongozwa na Sergio Aguero ambaye mpaka sasa amefunga magoli 10 katika mechi 10 za ligi nchini Uingereza.

Kikosi cha Manchester City kinaweza kuwa hivi: Hart; Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy; Milner, Fernando, Toure, Nasri; Dzeko, Aguero.

Rekodi kati ya QPR na Manchester City zinaonyesha kati ya michezo 44 waliyokutana QPR ameshinda michezo 12, huku City akishinda michezo 17 na wametoka sare michezo 15.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!