Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 November 2014
Thursday, November 13, 2014

Simba na Yanga sasa nikukomoana.


Na Oscar Oscar Jr

Watani wa Jadi timu za Simba na Yanga, wamekuwa ni watu ambao daima wataendelea kuteka hisia za wapenzi wa soka Tanzania kutokana na vituko, tambo na namna ambavyo kila mmoja wao anavyopenda kuwa mbabe wa mwenzie.

Usajili ni eneo ambao huleta mvutano mkubwa kwa timu hizi mbili, ni mara chache sana kupita dirisha la usajili bila timu hizi kongwe kuvutana. Simba wametangaza nia yao ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simoni Msuva na ada ya uhamisho ya mchezaji huyo inadaiwa kuwa Milioni 200.

Kabla ya Simba kumtaka mchezaji huyo, hapo awali Yanga walikuwa kwenye harakati za kumnasa Kiungo wa Simba, Jonas Mkude ambaye dalili za kumpata zimegonga mwamba baada ya kiungo huyo kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu yake ya Msimbani kwa kitita cha Milioni 60.

Simoni Msuva ni nguzo muhimu kwa sasa kwenye kikosi cha Yanga ambacho kipo chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo na tayari winga huyo ameonyesha kiwango cha juu huku akiwa mfungaji bora wa timu hiyo baada ya kutimiza magoli matatu kwenye mechi saba ambazo timu hiyo imecheza mpaka sasa.

Simba wameendelea kujitapa kuwa wako tayari kulipa gharama yoyote kwa mchezaji huyo huku Yanga wakisema wako tayari kumuuza mchezaji huyo kwa dau hilo na kama taratibu nyingine zitafuatwa. 

Simba na Yanga ni mwendo wa kukomoana tu. Mchezaji anaweza kuwa hafikii thamani hiyo lakini wapo tayari kumwaga pesa ili kumkomoa mpinzani. Dirisha la Usajili Tanzania bara litafunguliwa Novemba 15 na linatarajiwa kufungwa Desemba 15.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!