Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 November 2014
Saturday, November 15, 2014

Kocha ameamua Kurejea nyumbani


Na Chikoti Cico

Kocha wa zamani wa Manchester City na Galatasaray, Roberto Mancini arejea kuwa kocha mpya wa Inter Milan kwa mara ya pili baada ya kufukuzwa kwa Walter Mazzarri kutokana na mwenendo mbaya wa timu ya Inter kwenye ligi ya Italia maarufu kama SERIE A.

Inter Milan ambao wanashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 16 wamecheza michezo 11 na kushinda michezo minne, kutoka sare michezo minne na kufungwa michezo mitatu, Inter wamekuwa na mwenendo mbaya kwenye ligi huku wakipitwa kwa alama 12 na vinara wa ligi hiyo timu ya Juventus.

Mancini aliyeondoka Inter Milan mwaka 2008 baada ya kuiongoza timu hiyo kuchukua kombe la ligi ya Italia mara tatu mfululizo kati ya mwaka 2004-2008 anatarajiwa kurejesha ukali wa timu hiyo kwenye michuano mbalimbali ya ndani na nje ya Italia huku mechi yake ya kwanza kama kocha itakuwa dhidi ya AC Milan hapo Novemba 23.

Raisi wa Inter Milan Erick Thohir akiongea kwa furaha baada ya kumrejesha Mancini San Siro alisema “ Lengo letu ni kurejea kwenye nafasi yetu tunayostahili kama moja ya klabu kubwa Ulaya na ndiyo maana ninafuraha kumkaribisha tena Roberto Mancini, rekodi yake kwa Inter na sehemu zingine zinazungumza zenyewe, na uzoefu wake kimataifa na njaa ya mafanikio utaipeleka timu kwenye ngazi nyingine”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!