Searching...
Image and video hosting by TinyPic
12 November 2014
Wednesday, November 12, 2014

Boban sasa kuibukia Yanga.


Na Oscar Oscar Jr

Timu ya Yanga chini ya kocha Mbrazil, Maxio Maximo imemaliza mechi saba za kwanza ikijikusanyia pointi 13 baada ya kushinda michezo minne, kutoka sare mchezo mmoja na kufungwa mara mbili. 

Pamoja na timu hiyo kuwa na matokeo ambayo sio mabaya, wanachama na wapenzi wamekuwa hawaridhishwi na kiwango kinachoonyeshwa na timu hiyo uwanjani.

Yanga ya msimu uliopita ilikuwa inafanya vizuri sana lakini iliweza kuwapoteza viungo Frank Domayo aliyekwenda timu ya Azam na Athumani Idd Chuji, ambaye amekwenda Mwadui Fc ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza. Wachezaji hao ilikuwa nguzo ya kutengeneza mchezo wa burudani kwa Yanga.

Kwa mujibu wa Gazeti la Champion la leo, kocha Maximo anataka kuongeza nguvu kwenye safu ya kiungo ambayo kwa siku za hivi karibuni, amekuwa akitumika Mbuyu Twite na Hassan Dilunga ambao bado hawajaonekana kufanya vizuri katika idara hiyo na mchezaji, Haaruna Moshi Boban ametajwa kama mtu wa kuja kuchukuwa jukumu hilo.

Haruna Moshi msimu uliopita alikuwa na timu ya Coastal Union ya Tanga ambayo msimu huu, haikutaka kuendelea na kiungo huyo mshambuliaji. Pamoja na Boban, wachezaji wengine wanaowaniwa na Yanga ni Athumani Idd Chuji, Henry Joseph, Shabaan Nditi na Godfrey Bonny.

Kocha Maximo anaonekana kuvutiwa na wachezaji hao kwa sababu wengi wao anawafahamu kwani alikuwa nao kwenye timu ya Taifa wakati yeye akiwa kama kocha mkuu. 

Ligi kuu Tanzania bara imesimama kwa sasa huku dirisha la usajili likitarajiwa kufunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!