Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 October 2014
Friday, October 24, 2014

Uchambuzi: Tanzania Prisons vs Simba


Na Oscar Oscar Jr

Simba na Polis Morogoro ndiyo timu pekee kwenye ligi kuu ya Tanzania bara ambazo hazijaonja ladha ya ushindi msimu huu. 

Jumamosi hii Simba watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Maafande wa Jeshi la Magereza pale watakapo shuka dimbani Sokoine kusaka ushindi wao wa kwanza.

Baada ya mechi nne kupigwa, Simba amepata pointi nne na kujikuta kwenye nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu huku Tanzania Prisons, nao wakiwa na pointi nne kwenye nafasi ya tisa. 

Baada ya kuanza kwa ushindi ugenini mbele ya Ruvu Shooting, Prisons walijikuta wakichapwa na Jkt Ruvu nyumbani kwao wiki iliyopita.

Bado kocha wa Simba, Mzambia Patrick Phiri hajapata kikosi cha kwanza tangu kuanza kwa ligi kuu. Kila mechi ameonekana kubadilisha kikosi chake cha kwanza na gumzo ni wiki iliyopita dhidi ya Yanga alipoamua kumuacha nje mfungaji bora wa ligi kuu msimu uliopita, Amisi Tambwe.

Matokeo ya Tanzania Prisons msimu huu.

Ruvu Shooting 0-2 Tanzania Prisons
Yanga 2-1 Tanzania Prisons
Tanzania Prisons 0-0 Azam fc
Tanzania Prisons 1-2 Ruvu JKT

Matokeo ya Simba msimu huu.

Simba 2--2 Coastal Union
Simba 1-1 Polis Moro
Simba 1-1 Stand United
Yanga 0-0 Simba

Tanzania Prisons wamekuwa timu ambayo haitabiriki, mchezo huu wanacheza vizuri na mchezo mwingine wakivurunda. Walicheza vizuri dhidi ya Azam lakini hawakuwa bora mbele ya JKT Ruvu. Mara nyingi Prisons wanapokutana na Simba au Yanga, wameonekana imara hasa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Emmanuel Okwi bado ni aina ya mchezaji anayeweza kubadili matokeo muda wowote. Amehusika kwenye magoli matatu kati ya manne ambayo Simba wamefunga msimu huu. 

Ukitazama uwezo wake kwenye mchezo uliopita dhidi ya Yanga, ni wazi kuwa Okwi yuko kwenye ubora na Prisons, ni lazima wamdhibiti kama wanahitaji ushindi kwenye mchezo huo.

Huu ni mchezo ambao una presha kwa pande zote hizo  kwa sababu Prisons wamekuwa na matokeo mabaya hivi karibuni huku Simba nao, wakihitaji ushindi ili kushusha presha ya kocha, Viongozi na wachezaji. 

Uwezo wa Simba ni mkubwa lakini historia iko upande wa Tanzania Prison.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!