Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 October 2014
Monday, October 27, 2014

Ronaldo ashinda tuzo nchini Hispania.


Na Chikoti Cico

 Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno na Real Madrid Christiano Ronaldo anyakua tuzo ya mchezaji bora kwa msimu wa mwaka 2013/2014 kwenye ligi kuu ya nchini Hispania maarufu kama la liga. 

Tuzo hiyo imekuja baada ya Ronaldo kufunga magoli 31 kati ya mechi 30 alizoichezea timu ya Real Madrid kwa msimu uliopita.

Ronaldo ambaye pia alinyakua tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama “Ballon d'Or holder” kwa mwaka 2013 anakuwa mchezaji wa pili kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa la liga tangu kuanzishwa kwa tuzo hizo kwenye msimu wa mwaka 2008/2009 huku mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi akishinda tuzo hiyo mara tano toka ilipoanzishwa.

Zaidi ya tuzo ya mchezaji bora wa msimu pia Ronaldo alichukua tuzo ya mshambuliaji bora wa msimu na goli bora la msimu alilofunga dhidi ya Valencia kwenye wiki ya 36 ya msimu wa 2013/2014.
Baada ya kupokea tuzo hizo Ronaldo alisema “ Nahitaji kuwashukuru wachezaji wenzangu Real Madrid na familia yangu.

Huu ni wakati mzuri kwenye kazi yangu, kwangu kitu muhimu ni kushinda tuzo za pamoja ila napenda pia tuzo binafsi. Nafanya mazoezi kila siku kuendelea kuongeza tuzo zaidi kwenye tuzo hii”

Wakati Ronaldo akinyakua tuzo tatu kwa mpigo wengine walioweza kunyakua tuzo mbalimbali za msimu wa mwaka 2013/2014 ni kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone aliyechukua tuzo ya kocha bora wa msimu baada ya kuiongoza Atletico kuchukua ubingwa wa la liga huku kiungo wa Barcelona Andres Iniesta, akichukua tuzo ya kiungo bora mshambulaji wa msimu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!