Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 October 2014
Thursday, October 23, 2014

Mtendaji mkuu wa Chelsea aachia ngazi


Na Chikoti Cico


Mtendaji mkuu wa Chelsea aachia ngazi.
Mtendaji mkuu wa Chelsea kwa kipindi cha miaka 10 Ron Gourlay ameachia ngazi

Taarifa kwenye mtandao wa chelseafc.com inasomeka “ Klabu ya Chelsea inatangaza kwamba Ron Gourlay, baada ta miaka 10 ya mafanikio klabuni ikijumuisha miaka mitano kama Mtendaji Mkuu anaiacha Chelsea ili kuendelea na fursa mpya za kibishara”

“Klabu na hasa Mmiliki na Wakurugenzi, wanamshukuru Ron kwa miaka mingi ya huduma kwa Chelsea na tunamuunga mkono kwa hamu yake ya kutafuta changamoto mpya.

Juhudi za Ron zimeisaidia klabu kufanikiwa kwenye nafasi yake kama moja ya klabu kubwa duniani”

Kutokana na Gourlay kuachia ngazi mwenyekiti Bruce Buck na Mkurugenzi Marina Granovskaia wanatarajiwa kuongezewa majukumu zaidi ya kiutendaji mpaka hapo Mtendaji Mkuu mpya atakapoteuliwa.

Gourlay aliyejiunga na Chelsea mwaka 2004 na kufanya kazi kama Afisa Mtekelezaji Mkuu kabla ya kuchukua nafasi ya Peter Kenyon kama Mtendaji Mkuu mwaka 2009.

kabla ya kutua Chelsea, Gourlay aliwahi kufanya kazi Manchester United na kampuni ya Adiidas ambao ni watengenezaji wa vifaa vya michezo.

Ndani ya uongozi wa Gourlay Chelsea imeweza kunyakua kombe la ligi ya Uingereza, makombe mawili ya FA, Kombe la Europa na Kombe la klabu bingwa ya Ulaya lakini pia alihusika kwenye mazungumzo ya kumrejesha kocha Jose Mourinho kwa mara ya pili kwenye klabu ya Chelsea.

Gourlay akitoa shukrani zake alisema “Nimekuwa na fursa ya pekee kufanya kazi kwenye klabu na kuwa na mafanikio nje na ndani ya uwanja kwa miaka 10, ila najiskia muda umefika kuendelea na changamoto zingine.

“Ningependa kumshukuru Mr Abramovich, Wakurugenzi, Meneja na wachezaji na wafanyakazi wengine wote kwa kuniunga mkono kwenye kipindi changu ndani ya klabu, nawatakia mafanikio zaidi”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!