Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 September 2014
Tuesday, September 16, 2014

Alexies Sancheza kuibeba Arsenal Ugenini?


Na Oscar Oscar Jr

Arsenal leo itakuwa na kibarua kingine mbele ya timu ya Borussia Dortimund ya nchini Ujerumani pale timu hizo zitakapoumana kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya timu hizo pia kuumana kwenye hatua hiyo msimu uliopita..

Arsenal wanaingia kwenye mchezo huo huku wakimkosa mlinzi wao wa kulia Methieu Debuchy ambaye aliumia kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Manchester City uliomalizika kwa timu hizo kwenda sare ya kufungana mabao 2-2 kwenye dimba la Emirates na kijana Hector Bellerin anatarajiwa kuchukuwa nafasi hiyo ya mlinzi wa kulia.

Bado bingwa wa Dunia kiungo Mesut Ozil hajaweza kuonyesha uwezo wake kwenye mechi chache za ligi kuu ambazo amecheza mpaka sasa na hii inachangiwa na kocha wake Arsene Wenger kumpanga kama winga wa kushoto badala ya namba kumi mahari ambapo Ozil amekuwa akifanya vizuri.

Tangu kiungo huyo wa Ujerumani alipojiunga na timu hiyo ya London, kiwango chake kimekuwa ni cha kupanda na kushuka. Ubora wa Aaron Ramsey mara kadhaa umeonekana kumnufaisha sana na katika mchezo wao dhidi ya Manchester City, Ramsey hakuwa kwenye ubora wake hivyo haikuwa rahisi pia kwa Ozil kufanya makubwa.

Timu hizo zilikutana msimu uliopita huku Borussia Dortimund wakishinda Emirates Ugenini kwa mabao 2-1 na Arsenal akishinda 1-0 kule Sigunal Iduna Park. 

Alexies Sanchez anaonekana kama muhimili wa timu ya Arsenal kwa sasa baada ya kuongeza idadi ya mabao akiwa na arsenal pale alipofunga bao moja kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Manchester City.



0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!