Searching...
Image and video hosting by TinyPic
14 August 2014
Thursday, August 14, 2014

Makocha wazawa wanarudisha nyuma soka la bongo


Na Gaucho wa Kalamu

Unapofanya jambo lolote kwa kipindi kirefu na ukaona hakuna mafanikio yanayoonekana au hata yale ya kufikirika ni lazima ufanye tahmini ni kitu gani kinafanya mambo kwenda mlama kiasi hicho. Kwa kipindi kirefu sasa nchini Tanzania tumekuwa na ligi kuu ya mpira wa miguu ambao imechezwa kwa muda mrefu  sasa.

Pamoja na ukongwe wa ligi yetu bado mafanikio katika soka la ndani na la kimataifa yamekuwa changamoto kubwa sana.

Ligi imekuwa ikiendelea kukumbana na matatizo yale yale kila kukicha kiasi kinachofanya hata timu yetu ya taifa kukosa uimara katika mashindano mbalimbali tunayoshiriki.

Tathmini mbalimbali zinafanywa na kushindwa kuelezea ukubwa wa tatizo letu huku tathmini nyingi zikitoa sababu zinazofanana ambazo binafsi naamini sio mwarobaini wa soka letu.

TFF kama chombo cha kuendeleza soka hapa nchini, kina kazi kubwa sana kuhakikisha inafanya ligi yetu inakuwa bora kwa kila uwezekano.

Kuna vitu vya msingi ambavyo TFF inatupia lawama klabu lakini matatizo ambayo kwangu nayaona makubwa kama vile Viwanja vibovu, waamuzi wabovu na mipango endelevu ya soka nadhani ipo ndani ya uwezo wa TFF.

Baada ya kutafakari nikagundua kuna tatizo kubwa sana katika ligi yetu, na hili ni kubwa zaidi lakni tunaliona la kawaida maana watanzania tumeumbwa na roho za kukata tamaaa na kuamini katika sababu ambazo hazina ukweli hata robo.

Ntaeleza sababu KUMI za msingi kwanini soka letu halikuwi tukianzia katika ligi kuu hadi tiu za taifa.Sababu hizi nimezipanga kutokana na nyakati na mafanikio yaliyopatikana kwa mtazamo wa ligi na timu ya taifa.

1. MAKOCHA/WAALIMU/WAKUFUNZI

Tumekuwa na lundo la waalimu ambao hawana mafanikio yanayoweza kupimwa kwa macho zaidi ya mafanikio ya historia yaliyojaa sababu za uongo ambazo ndani yake hazitujengi.

Waalimu wengi wanaofundisha soka Tanzania ni wale wale wa kila siku ambao mafaniko yao hayapimiki hata kwenye mzani.

Waalimu hawa wameshindwa kufungua hata mipaka kwenda kujaribu kujifunza na kupata changamoto mpya katika ligi za nchi jirani ila wamebaki kuganda nchini.

Kuna makocha wanaonekana wao ni wa ligi kuu na makocha wanaonekana kazi zao kuzipandisha timu ligi kuu.

Hawana maendeleo kwenye Tasnia yao na hapo ndio akili na mawazo yao yamegota. Majina kama Othman Mumba, Charles Kilinda, Jumanne Challe, Mbwana Makata, Hassan Banyai, Fred Minziro, Jamhuri Kihwelo, Abdalah Kibadne, John Simkoko, yamekuwa si mageni kwenye masikio yawapenda soka hapa Tanzania.

Hawa makocha wote ukimuondoa John Simkoko ambaye aliipa ubingwa wa Tanzania Bara Mtibwa Sugar hakuna aliyewahi kushinda ubingwa huo akiwa na klabu tofauti na wakongwe Simba na Yanga.

Wakati msimu uliopita ukimalizika, Abdallah Kibadeni alikuwa katika hekaheka za kuibakisha ligi kuu timu ya Ashanti United wakati Jamhuri Kihwelo aikihangaika kuipandisha timu ya mwaduni Shinyanga ligi kuu.

Habari za Charles Kilinda atimuliwa Jkt Ruvu na habari za Mbwana Makata apewa Ulaji Mgambo JKT si ngeni masikioni mwetu. Habari za Fred Minziro afungishiwa virago Yanga zimekuwa kama Tamthilia masikioni mwetu.

Najaribu kujenga picha juu ya makocha hawa wazoefu ambao wametawala katika ligi kuu lakini wanashindwa kujenga kitu kipya kwenye historia ya maisha yao kama makocha.

Hawa ndio naweza kuwataja kama sehemu ya kwanza ya kufeli kwa mafanikio ya timu nyingi hapa nchini.

Wanazidiwa kwa hali ya juu uwezo na wachezaji wanozalishwa hapa nchini. Nchi yetu imekuwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu lakini hatuna makocha wanaoweza kuvitumia vipaji hivyo na kuweza kuleta mafanikio.

Hawa makocha wamekuwa wakibadilishana timu tu kama kupanda bus pale Ubungo. Leo huyu utamkuta African Lyon, mwingine utamkuta Prison ya Mbeya. Kesho utamkuta Ruvu Shooting na mwingne utamkuta Kagera Sugar.

Wote ndani yao wana mafanikio ya kusaidia timu isishuke daraja au kuipandisha timu ligi kuu. Hawana ndoto za kuchukua Ubingwa ndani ya akili zao.

Usione ni wajinga wale Viongozi wa timu kubwa wanaoamua kuchuka makocha kutoka nje ya nchi, wanatambua fika changamoto za makocha wa Kiswahili ambao mafanikio yao kwao yamekuwa ni ndoto ila wanafanya kazi za ukocha ili kupata hela ya kula na sio kupata mafanikio ndani ya maisha yao.

Ni dhahiri vipaji vingi vinavyoibuliwa na makocha hawa ni zaidi ya uwezo wa hawa makocha. Kocha bora ni Yule anayeweza kumjenga mchezaji katika mfumo wake.

Hilo ndio tatizo kubwa na katika hali ya kawaida huwa nasema wachezaji wote wa Tanzania wana viwango vinavyoshabiana ila wanatofautiana kutokana na changamoto wanazokumbana nazo ndani ya klabu zao.

Hawa makocha ndio sumu ya kwanza ya maendeo ya soka nchini. Unajua sumu nyingine ni nini? Usikose kusoma sehemu ya pili ya Makala hii..

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!