Searching...
Image and video hosting by TinyPic
11 April 2014
Friday, April 11, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI CHACHA KUCHEZESHA MICHUANO YA AYG


Na Boniface Wambura


Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua mwamuzi msaidizi wa Tanzania anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ferdinand Chacha ameteuliwa kuchezesha michezo ya Vijana ya Afrika (AYG- African Youth Games).

Michezo hiyo ya kwanza ya Afrika itachezesha jijini Gaborone, Botswana kuanzia Mei 22-31 mwaka huu. Tanzania pia itashiriki katika mashindano hayo ya vijana wenye umri chini ya miaka 15.

SIMBA, ASHANTI UTD KUVAANA TAIFA
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho(Aprili 12 mwaka huu) katika raundi ya 25 ambapo Simba na Ashanti United zitapambana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Mechi nyingine zitakuwa kati ya Tanzania Prisons na Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya) wakati Coastal Union itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Keshokutwa (Aprili 13 mwaka huu) kutakuwa na mechi nyingine nne za kukamilisha raundi hiyo.

 Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya wenyeji Oljoro JKT na Yanga. Mtibwa Sugar itacheza na Ruvu Shooting (Uwanja wa Manungu, Morogoro), Mgambo Shooting na Kagera Sugar zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mbeya City ikiumana na Azam kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!