Searching...
Image and video hosting by TinyPic
5 April 2014
Saturday, April 05, 2014

SHOMARI KAPOMBE KUTUA AZAM FC



AZAM FC inahaha kila kona kuhakikisha beki Shomari Kapombe anatua katika himaya yao tayari kwa ajili ya kumtumia katika msimu ujao na imeweka mezani ofa ya maana kumnunua beki huyo kutoka AS Cannes ya Ufaransa.
Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Ufaransa asubuhi jana (Ijumaa), wakala wa beki huyo Dennis Kadito alisema, Azam imekuwa katika jitihada kubwa za kuhakikisha inamsajili mteja wake huyo, ambapo awali kupitia kwa Yusuf Bakhresa walituma ofa ya Euro 40,000 (Sh milioni 88) ambazo ziligomewa na Wafaransa hao.
Kadito  alisema Cannes baada ya kugoma, Azam waliwatajia kiasi ambacho wanakihitaji ili kumuuza beki huyo ambacho ni Euro 70,000 (Sh milioni 154) na Yusuf ambaye pia ni wakala wa kuuza wachezaji alikubali kulipa.
Inadawa kwamba, Azam walikubali kulipa kiasi hicho baada ya kugundua wameshafanya makosa ya kumshawishi Kapombe avunje mkataba wake na Cannes na beki huyo tayari ameshawasilisha barua ya kufanya hivyo tangu Februari 27, mwaka huu.
“Nilipigiwa simu na Yusuf ambaye alitaka kumnunua Kapombe ili asajiliwe Azam FC kwa kiasi hicho cha Euro elfu 40 lakini kikakataliwa na Cannes ambako wanataka elfu 70,Yusuf hakukubali akasema ataangalia jinsi ya kutumia sheria kumpata Kapombe.
“Baadaye Kapombe alituma barua Cannes akitaka mkataba wake na klabu hiyo uvunjwe, barua hiyo iliandikwa na mchezaji mwenyewe lakini ukiichunguza kwa makini ni wazi kwamba alipata msaada kutoka kwa wanasheria,” aliongeza Kadito licha ya kwamba Yusuf hakupatikana jana kutoa ufafanuzi wa suala hilo.

source:Gazeti la Mwanaspoti.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!