Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 April 2014
Wednesday, April 23, 2014

MAN UNITED YAJIPANGA KUSAKA MRITHI WA DAVID MOYES




Meneja David Moyes amepigwa chini na Manchester United, klabu hiyo imetangaza siku ya Jumanne baada ya msimu wake wa kwanza kugeuka kuwa janga kubwa kwa magwiji hao wa Uingereza.

“Manchester United wanatangaza kuwa David Moyes ameondoka kwenye klabu hii,” United walichapisha kwa anwani yao rasmi katika mtandao wa kijamii wa Twitter.
“Klabu hii kingependa kumshukuru kwa bidii, uadilifu na unyofu alioleta kwa wadhifa wake.” 

Habari za kutimuliwa kwa Moyes zilijili baada ya vyombo vya habari Uingereza kutangaza kuwa utawala wa miezi 10 wa Moyes unayoyoma baada ya kumrithi gwji Sir Alex Ferguson aliyestaafu musimu uliopita. 

Raia huyo wa Scotland, 50, amejikuta kwenye balaa moja hadi nyingine huku United, mabingwa wa ligi ya Premier wakishuka hadi nafasi ya saba na kuchakazwa kwao 2-0 na Everton Jumapili kulidhibitisha hawatafuzu kombe la mabingwa kwa mara ya kwanza tangu 1995. 

United wako alama 13 nyuma ya nafasi ya nne na 23 nyuma ya wapinzani wao Liverpool wanaopigiwa upatu kuwarithi kama mabingwa wa Premier ikisalia mechi nne muhula huu kumalizika.

Kulingana na duru, afisa mkuu mtendaji wa United, Ed Woodward, alimuarifu Moyes binafsi uamuzi wa kumpiga chini katika makao yao ya Carrington Jumanne asubuhi. 

Mkongwe Ryan Giggs na mwenzake Nicky Butt wanatarajiwa kuchukua hatamu za uongozi kwa muda na kuongoza United dhidi ya Norwich City Jumamosi huku miamba hao wakisaka mrithi ambaye atarejesha hadhi yao. 

Louis van Gaal, kocha wa Uholanzi, amepigiwa upatu na wadau kuchukua wadhifa huo huku Jurgen Klopp (Borrusia Dortmund), Diego Simeone (Atletico Madrid) na Giggs wakitajwa kama wengine wanaowazwa na bodi ya klabu hiyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!