Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 April 2014
Friday, April 04, 2014

CHRISTIANO RONALDO NA UTATA WA JERAHA LAKE.



 Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Licha ya kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti kusisitiza kwamba hamna haja ya kuwa na wasiwasi kutokana na kuchechemea kwa Cristiano Ronaldo mwishoni mwa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano, tukio hilo lazima litaibua wasiwasi Ureno. 

Nahodha huyo wa timu yao ya taifa, mfungaji mabao anayeongoza La Liga na Ligi ya Mabingwa msimu huu, atahitaji kudumisha ufungaji mabao wake kuhakikisha Ureno wanasonga kwenye fainali za Kombe la Dunia Brazil ambazo zitaanza Juni. 

Hata hivyo, mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United mwenye miaka 29, amekuwa akilalamikia uchungu kwenye goti lake la kushoto wiki za hivi majuzi na amekuwa akicheza akiendelea kupokea matibabu kutoka kwa matabibu wa Real. 

Alifunga bao lake la 14 na kufikia rekodi ya Ligi ya Mabingwa msimu huu wakati wa ushindi wao wa 3-0 robofainali, ushindi wa mechi ya kwanza wakiwa nyumbani dhidi ya Borussia Dortmund kabla yake kuomba aondolewe uwanjani dakika 10 kabla ya mwisho wa mechi. 

"Ni tatizo ndogo la goti na sina wasiwasi,” Ancelotti alikiambia kikao cha wanahabari.
“Kama tatizo hilo, ambalo kwa sasa halizui wasiwasi, litaendelea, basi tunaweza kumpumzisha mchezaji huyo,” akasema Mwitaliano huyo. 

“Nilimuondoa dakika 10 kabla ya mwisho wa mechi na hamna haja ya wasiwasi.”
Real wana mechi nyingi za kucheza wiki hizi za mwisho za msimu na wana mechi kali dhidi ya Real Sociedad walio wa sita ligini Jumamosi kabla ya mechi ya marudiano Jumanne Dortmund. 

Mapato ya klabu hiyo tajiri duniani bado yanatiririka na wana nafasi ya kushinda mataji matatu msimu huu, ingawa kushindwa kwao La Liga na Barcelona na Sevilla mwezi jana kulipelekea wao kuteleza na kujipata wakiwa nambari tatu nyuma ya Atletico Madrid na Barca.
Watacheza dhidi ya Barca, ambao wamewashinda nyumbani na ugenini kwenye La Liga msimu huu, katika fainali ya King's Cup Aprili 16.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!