Searching...
Image and video hosting by TinyPic
31 March 2014
Monday, March 31, 2014

TON KROOS KUJIUNGA NA MAN UNITED.


Mwenyekiti wa timu ya Bayern Munich  Karl-Heinz Rummenigge ameendelea kusisitiza kuwa kiungo mshambuliaji Toni Kroos hawezi kujiunga na Manchester United msimu ujao. 

Kiungo huyo 24 bado hajasaini kuongeza mkataba wake ambapo huu wa sasa,unatazamiwa kumalizika mwishoni mwa msimu wa mwaka 2015, hii yote ni kwa sababu kuna picha mabazo zilisambaa zikimuonyesha kocha  David Moyes akiwa pamoja na mchezaji huyo na wakala wake kipindi kocha huyo wa United alipokuwa ziarani nchini Ujerumani mwezi januari mwaka huu.
 

Mapema mwezi huu Kroos alikaririwa kutokupinga uwezekano wa yeye kujiunga na United,lakini kwa sasa Bayern wameibuka na kudai kuwa,kiungo huyo hatoruhusiwa kuondoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

"Toni Kroos anauhakika kuwa atakuwa akiitumikia Bayern Munich msimu ujao" Rummenigge aliwaambia wanahabari siku ya jumatatu.

Kroos amekataa kuweka wazi juu ya kujikita Bayern alipoulizwa kuhusu mkataba wake alisema “kila kitu kinawezekana”  na hii ilitokana na swali la kama atakuwa tayari kujiunga na timu ambayo haitoshiriki klabu bingwa Ulaya msimu ujao.

“Nimeshagundua kuwa mengi sana yameandikwa kuhusiana na hilo.Sioni kama  kuna jambo jipya.Hakuna uamuzi wowote ambayo umeshachukuliwa.bado hakuna makubaliano yoyote,” Kroos alizungumza mapema mwezi wa machi.


"Jambo hilo litabakia kama lilivyo mpaka mwisho wa msimu,uamuzi utafanywa.Hakuna usiri wowote Man United wanaonekana kunihitaji." alisema Kroos

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!