Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 March 2014
Sunday, March 30, 2014

MGAMBO WAIFUNGA YANGA BAO 2-1 HUKO TANGA



Young Africans leo imepoteza mchezo wake wa pili katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kufungwa kwa mabao 2-1 na wenyeji timu ya Mgambo Shooting ya Handeni katika mchezo uliofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Mgambo walijipatia bao a kwanza dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wake Fully Maganga ambaye aligongwa na mpira huo kabla ya kujaa wavuni kufutia mlinzi Kelvin Yondani kumrudishia mlinda mlango wake Juma Kaseja mpira na wakati akiupiga mbele ukambabatiza mfungaji.

Baada ya bao hilo Young Africans ilifanya mashambulizi mfululizo langoni mwa Mgambo JKT lakini ilikuta mipira ikigonga miamba na kuokolewa na walinzi wa Mgambo huku mipira mingine ikiokolewa nakuwa kona ambazo hazikuzaa matunda yoyote.

Dakika ya  30 mwamuzi wa mchezo wa leo Alex Mahagi alimtoa nje mshambuliaji wa Mgambo JKT Mohamed Neto kufuatia kukutwa amefunga hirizi kwenye bukata jambo ambalo lilileta tafrani uwanjani na mchezaji huyo kutolewa huku akizomewa na wapenzi wa mpira waliokua wamejazana uwanjani

Yanga waliendelea kulishambulia lango la Mgambo JKT bila mafanikio kwani mipira yao ilikuta ikiondolewa na walinzi  na mlinda mlango wao.

.Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza, Mgambo JKT 1 - 0 Young Africans
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kucheza kwa kasi na katika dakika ya 50 Nahodha wa Young Africans Nadir Haroub "Cannavaro" aliipatia timu yake bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Mgambo JKT kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Dakia ya 69 ya mchezo, uzembe wa mlinzi wa Kelvin Yondani uliigharimu Young Africans baada ya kumchezea madhambi mshambuliaji wa Mgambo JKT ndani ya eneo la hatari na mwamuzi kuaamuru penati ambayo ilipigwa na Malima Busungu na kuipatia Mgambo bao la pili.

Young Africans iliendelea kushambulia kwa kasi kusaka bao la kusawazisha lakini bado ukuta wa Mgambo JKT uliendelea kuonekana imara sana na ngome yake kushinda kupenyeka.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Mgambo JKT 2 - 1 Young Africans.

Young Africans: 1.Juma Kaseja, 2.Mbuyu Twite,  3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub "Cannavaro", 5. Kelvin Yondani, 6.Frank Domayo, 7.Saimon Msuva/Hamis Kizza, 8.Hassan Dilunga, 9.Didier Kavumbagu 10.Mrisho Ngasa/Hussein Javu, 11.Emmanuel Okwi

Taarifa hii ni kwa mujibu wa website ya YANGA.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!