Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 June 2013
Sunday, June 09, 2013

TUSKER FC WAMEGOMA KUSHIRIKI cecafa


by George Otieno    

Klabu ya Tusker FC ya hapa Kenya,mabingwa mara tano wa CECAFA,1988,1989,2000,2001 na 2008,wadinda kushiriki kwenye dimba la klabu bingwa kule Sudan.Sababu haswa ikiwa ni hali ya usalama kwa wachezaji wake.

Hii simara yakwanza kwa klabu hii kujiondoa kwenye mchuano huu kongwe Barani Afrika.Mwaka wa 1979 pia walidinda kushiriki kwenye mchuano wa CECAFA iliyoandaliwa nchini Somalia,sababu zikiwa ni usalama.Lakini Kenya iliwakilishwa na AFC Leopards ambao walinyakua ubingwa walipoilaza klabu ya Kampala City Council kwa bao 1-0.

Kama Tusker watadinda basi Kenya itawakilishwa na Gor Mahia"Kogalo"ambao nimabingwa mara tatu wa kombe hili,1980 wakishinda watani wao wa jadi AFC Leopards kule Malawi kwa bao 3-2
Hadi sasa hamna fainali kali kama hii ya Blantyre,1981 walishinda Simba"wekundu wamsimbazi"hapa Kenya kwa bao 1-0 na mwaka wa 1985 walibwaga tena watani wao wa jadi AFC Leopards kwa bao 2-0 nchini Sudan.

kumbuka Gor Mahia walishinda Leopards nakikosi cha pili,kwani baadhi ya wachezaji wa Gor walipigwa marufuku na CAF baada ya kuzua kizaza nchini Misri walipochuana na Zamalek.Hadi sasa katika historia ya CECAFA huo ndiyo ulikuwa ushindi wa uchungu zaidi,kwani AFC walirudisha kombe baada ya kuishinda Gor mwaka wa 1984 hapa Nairobi kwa bao 2-1,lakini Gor Mahia ikarudi na kikombe,jambo la kuudhi wachezaji wote walitumia ndege moja kutoka Sudan.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!